Nadhari juu ya Neema na Sheria

Na: Peter Youngren
Kutoka: November 2008
Patikana ndani ya: Injili ya Neema
Fikira kumi kwa ajili kutafaghari kwako juu hili somo la muhimu

Nina amini katika Sheria na makusudi iliyo weza kufanya iletwe: sio kwa kuokoa,kuponya au kutufanya watakatifu, lakini ni kutuonyosha hitaji letu la mwokozi.Sheria ya Musa ilikuwa ni ya kipindi cha miaka elefu moja na mia nne iliyo tuonyesha ya kwamba hakuna anayeweza kuwa mwenye haki kwa matendo. Hivyo ndivyo sheria ilivyo- matendo ya mwanadamu kupendeza Mungu asiye furahia. Dini zote zipo juu ya msingi wa mchezo ya mwanadamu, na la kuhuzunika wengi wanapunguza Ukristo kuwa dini ya matendo. Ukristo bila Injili Ya Neema ya Mungu(Mtendo 20:24) Sio nzuri kuliko dini ingine yeyote.

Sheria ni yale tunaweza kufanya au, kutenda na jitihada letu. Inatenda kazi kwa mambo ya inje,kuweka uweza wetu katika kuonekana. Neema ya Mungu ni kitu usicho hesabiwa, usio fanyia kazi, kibali ambacho hauhitaji kupata. Kibali hiki kipo juu ya msingi wa utendaji wa Yesu, kazi Yake iliyo kamilika msalabani na uweza Wake wa kuokoa,kuponya nakutakasa wao “ wana kuja kwa Mungu kupitia Yeye” (Waebrainia 7:25)

Nime ongezea Fikira kumi kwa ajili ya kutafaghari kwako juu ya somo hili lilo muhimu. Ruhusu Roho Mtakatifu aangazie yale Yesu amekufanyia wewe.

1. Sababu na makusudi

Dini ya Sheria iliyo juu ya msingi wa matendo yetu itatufanya kutenda mambo mazuri, lakini katika sababu mbaya.Maombi, Kujisomea Bibilia, kutoa na kushuhudia yote ni mambo mazuri,walakini yata tufaidi iwapo tutatenda katika kazi ya Yesu iliyo kamilika msalabani. Paulo anatuambia ya kwamba iwapo tunaweza kutoa pesa zetu zote kwa maskini, lakini hatuna upendo, haitatufaidi chochote (1 Wakorintho 13:3 ), Kwa uhakika vipawa vyetu vita faidi maskini sawasawa, tukitoa pasipo upendo au hamna. Walakini Baba wa mbinguni unatupenda sana kwamba anataka tufaidike.

Tufanyapo mambo mazuri ilitufarahishe Mungu au watu, haya mambo mazuri hayatufaidishi kitu. Kwa upande mwingine, tunapo itikia upendo wa Mungu kwa kupenda wengine,haya ni matendo mema ambayo yata dumu. Wafarizayo, wa miako 2000 awali na wa sasa,wote wanahusika sana jinsi wanavyo ona wengine.Yao inahusu kutunza kuonekana kwa inje, haswa kushangaza wanaoshiriki kanisa lile moja, walio na sheria za nakala za namna hiyo ya lilo lema na mbaya tunayofanya. Neema inahusu kufurahia yale Yesu ametendea sisi, na kuitikia upendo Wake kwa kutembea katika yaliyo wekwa wakfu awali “ matendo mema” Aliye tuumbia. (Waefesso 2:10)

2. Uzuri wa kidini au uaminifu

Wakati mwingine wanawake wanapo jipamba manukato yao wao huita “kujivika uso wao.” Sheria ni dini iliyo mzuri- kujivika uso mzuri wa Kikristo. Yesu alimwambia mwanamke Msamaria “Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.” (Yohana 4:23)

“ Tunapo fanya mambo mzuri kupendeza Mungu, haya matendo mzuri hayatufaidi chochote.”

Katika “Roho” inamaanisha Agano Jipya, ni agano la Roho, ambalo lina simama ukilinganisha agano la andiko (2 Wakorintho 3). Agano la kwanza hutoa uzima na la pili hua. Katika “Kweli” inamaanisha kwa uhakika.Agano la kale lilikuwa la umbo la inje,Mungu aliye inje, na Agano Jipya la tenda kazi kwa wanaoabudu kwa kweli, Mungu aliye ndani. Neema inatuwezeza kuwa kweli na waaminifu.Sio sifa njema iliyo katika mambo yanayo amua. Lakini ni utendaji ulio kamili wa Kristo unaojalisha.Mungu hakupendi sio kwa yale umemfanyia Yeye ila ni kwa yale Yesu alifanya kwa ajili yetu pale msalabani. Hakuna hitaji la kujifanya, kuji “vika nyuso zetu.” Iwapo kuna ukosefu ndani yetu,ruhusu ionekane mahala ambako tunaweza ruhusu upendo wa Mungu kutusaidia sisi.

3. Jawabu la ukosefu wetu

Sheria ya kidini katika maumbile yake yote iko na mambo fulani ya kimisingi. Kila wakati kuna sheria ingine yakuitekeleza, jugumu ingine kwetu kuitimiliza,zaidi ya tabia ya uungu ya kuijenga, na kila wakati shida ingine ya kibanafsi inayo tuhitaji kutubu toka kwayo- katika hali hiyo sisi hatukuwi bora kamili.

“ Dhambi zetu ziwe kubwa au ndogo katika machoni pa watu, sisi sote ni sawa tunahitaji Yesu.

Iliyopo hapo ikiwa kweli, Injili ni kwamba Yesu huridhisha mambo ya haki yanayohitajika ya Sheria kwetu sisi.Alitimiza yote yaliyo hitajika, na tabia ya utaua ya kweli huimarishwa na Kristo anayeishi ndani mwetu. Tabia njema haziji kwa kuangalia wema adilifu ila ni kwa Kristo aishiye ndani. “Na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha haya ninayoishi sasa naishi kwa imani, imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu.”(Wagalatia 2:20) Ni ukubwa gani una ruhusu Yesu kuwa ndani yako?

4. Je ni vipi kuhusu matemdo mema?

Katika kilindi cha Sheria ya kidini ni kusadiki ya kwamba tukijaribu kwa nguvu, kuomba zaidi,na kufanya zaidi,tutalazimisha Mungu kutupa sisi msamaha zaidi, baraka, uponyaji au ustawi.Hili ni funzo la walio bora zaidi ambalo linatupa sisi utukufu, na sio Kristo. Hii fikira husimama na kulinganisha kuamini yale Yesu amefanya,jinsi ilivyo nukuliwa katika wimbo.” Juu ya Yesu aliyo mwamba imara,ila udongo mwingine ni mchangana uangukaye.” Sheria ya uhalilisho hutuambia tuwe zaidi ya haki, bora, fanya kazi kwa bidii,jingozea maisha yako,toa zaidi, tumika zaidi, fanya zaidi.Injili ya kubali ya kwamba Kristo ameweka maisha Yake ya uumbaji ndani mwetu.” Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.” Matendo mema sio matokeo ya bidii na makusudi, lakini ni matokeo yake ni kutambua kwanini tulizaliwa mara ya pili. Tuliumbwa kwa ajili ya “ matendo mema” katika Kristo Yesu.

5. Unafiki au uhakika

Katika mathayo 15 tuna soma hadithi ya Mfrisayo aliye onekana kuwa mkubwa kwake wanafunzi wa Yesu maana walihusika katika desturi iliyo wekwa ya kusafisha na kujitawaza mikono kabla ya kula,ila wanafunzi wa Yesu hawakufanya hivyo.Wafarizayo walitumia shilindano kumhukumu Yesu na wanafunzi wake.Lakini Yesu aliwaweka wazi kuwa ni walaghai wa rohoni. Maana wao wali “chokoa tunda” moja ya amri na wakatumia kumhukumu Yesu na wanafunzi wake,na wao wenyewe walikuwa na hatia ya kuvunja amri zingine zilizo kuwa mzito.Unaona sheria ita zaliza utundu na adabu. Soma hadithi hiyo yote katika mathayo 15:1-10.Ni mchezo nyimivu kati ya Yesu na baadhi ya wanafiki wa rohoni wakubwa ambao wali wahi ishi. Neema inasimama dhidi ya sheria maana inazalisha ukweli. Unaishia jinsi ulivyo. “Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika.” 2 Wakorintho 5:17).Unapokuwa unafurahia uumbaji mpya wa maisha ndani yako, hauna chochote cha kutafuata wengine makosa, badili yake una lenga kushiriki maisha mapya ambayo umepokea.

“Tunapo kubali ya kwamba Yesu pekee ndiye safi,tunajipata wenyewe tunatubu haki yetu ya kibinafsi na kujitegemea wenyewe.”

6. Je sisi tuna ona hitaji la Yesu kwetu?

Katika Luka 7 tunaye hadithi ya mwanamke mwenye “dhambi” akiabudu Yesu nyumbani mwa Mfarisayo kwa jina Simoeni. Dhambi zake zilikuwa dhairi na kujulikana katika jamii ; kwa hakika alikuwa kahaba. Dhambi za Simeoni hazikutambulikana sana :kiburi, haki ya kibinafsi,utundu na unafiki. Tuna soma kuhusu Yesu akikabiliana na hawa wawili, tuna tambuwa ya kwamba Kristo hapakuwi dhambi moja toka kwa ingine. Katika macho ya Mungu dhambi ni dhambi.Katika yote, Simon alikuwa dhambi mbaya sana kwa sababu ya haki ya kinafsi iliyo funika mtizamo wake wa rohoni. Hakuona uhitaji wa Mungu kikamilifu.Badala yake aliangalia wengine ndio wanalo hitaji, ili hali akijiona mwenyewe kuwa safi.
Mara tukikumbatia Injili ya Neema, semi zetu zita shangilia zile za Mtume Paulo “Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu” Japokuwa dhambi zetu ni kubwa au ndogo machoni pa watu zote tunahitaji Yesu.

7. Usomi wa rohoni au sawasawa tuna uhitaji

Usomi wa rohoni ni mtego mbaya ambao ume watega wengi katika historia yote. Mmoja aliye tegwa katika mtego huu ni Simeoni, yule Mfarisayo ambaye nyumbani mwake Yesu alitembelea. Hadithi katika Luka 7 ina tuonyesha watu wawili ambao wako kinyume na mwengine. Yule mke alikuwa ame julikana kwa maisha uasherati ; na Simoeni alikuwa na tabia njema iliyo julikana. Simoeni anaonekana kama hakujiuliza swali kama “ Je ni dhambi kiasi gani unahitaji kutenda ndiposa uwe mwenye dhambi?” Yesu analete jawabu kwa swali hili, baadaye akikubaliana na mtume Paulo kwamba ukipatikana na hatia katika moja basi una hatia katika yote.

“ Usi kate tamaa kwa Mungu- Yeye haja kata tama kwako!”

Fikiria watu wawili wanalo hitaji ili maisha yao yaokolewe lazima waruke magenge marefu ya Moto Makubwa.Mmoja ni mwanaridha wa Olimpiki aliye shinda medali ya dhahabu katika kuruka, na yule mwingine ni mfanya biashara mzee ambaye haja wahi kufanya mazoezi hata siku moja maishani mwake. Bila shaka yule mwana olimpiki atafanya vizuri zaidi kuruka kuliko huyu mfanya biashara, lakini mwishowe wote watakuwa na ajali moja - chini ya Magenge marefu ya Moto. Hii ndiyo lengo la hili Andiko, linayo tuambia ya kwamba wote wametenda dhambi na wame pungukiwa na utukufu wa Mungu, lakini karama ya uzima wa milele ni kwa neema kwa yoyote aminiye (Warumi 6:23).Hakuna aliye na chochote juu ya mwingine; pale msalabani sisi sote tu sawa.

8. Je hii ni neema ya kuchukiza?

Neema haileti maana. Ni ya kuchukiza machoni pa watu wengi. Kwa nini Mungu aweke gadhabu yake juu ya Yesu? Kwa nini Yesu alitaka alipe deni ambalo halikuwa lake? Kwa nini mzigo huu wa deni ulipwe kabla wewe na mimi hatuja zaliwa? Na kuiongeza kabisa, kwa nini Mungu ana tupa huu msamaha kama karama iliyo bure? Na baada ya yote, ingekuweje iwapo tungechukuwe faida ya upendo wa Mungu usio na sharti? Jambo hili kwamba anatupa wokovu, bila masharti, je si hii ni chukizo? Ni vipi Mungu anasema kwamba msamaha utolewe sabini mara saba kila siku?

Ndiyo upendo wa Mungu ni chukizo jiwe likwasalo kwa nia ya kifarisayo na ujinga ya msomi wa kidini, lakini kwetu sisi tunao amini, ni nguvu na hekima ya Mungu. Ni neema Yake inayo tusababisha kutawala katika maisha na kushinda majaribio na mitego, na kuishi kwa kujitolea na takatifu kwa ajili ya Yesu (Warumi 5;17, 1Wakorintho1:18-25, Tito 2:11, 12).

9. Ni nani anaye pata utukufu?

Mara nyingi watu hawataki habari njema ya neema ya Yesu, sana sio mara ya kwanza. Wanadamu huwa hasherekei neema ya Mungu. Juu ya yote iwapo tuta pokea,yasio ya bidii,kibali isiostahili ya Mungu itolewayo kupitia Yesu Kristo, basi hatuwezi kuchichukulia sifa yoyote kwetu sisi.Ina maanisha wokovu wetu na baraka zote zinazo kuja ni kwa sababu ya kazi iliyokamilika ya Kristo msalabani, na sio matendo yetu, hakuna utukufu kwetu, yote ni kwake Yesu.
Injili ya neema inasimama katika ulinganisho ulio ngumu juu ya dini zote, ambayo inahusu mambo tunayo weza kufanya. Neema inahusu yale Yesu amefanya.Tunapo kubali Yesu pekee yake ametosha tunajipata wenyewe tuna tubu haki yetu ya kibinafsi na kujitegemea.Hapo kitu cha a jabu hutokea – tuna anza kufaulu na kuruka juu kwa mapawa maishani kwa sababu nguvu zilizo ndani za neema Yake. Hicho ndicho kilicho vuta mtume Paulo kwa ukuu.Aka andika, “Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.” (1 Wakorintho 15:10)

Mara tukikumbatia Injili ya Neema, semi zetu zita shangilia zile za Mtume Paulo “Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu” Japokuwa dhambi zetu ni kubwa au ndogo machoni pa watu zote tunahitaji Yesu.

10. Upendo na neema ya Mungu haikomi!

Usi kate tamaa kwa Mungu- Yeye haja kata tamaa kwa ajili yako! Tukisoma safari ya Waisrael kupitia jangwa wakati mwingine ina shusha moyo, na bado hadithi hiyo iko na mambo mengi yanayo himiza. Sehemu ishushayo ni kwamba Israeli wange ingia katika nchi ya ahadi haraka mno, labda katika majuma 3-4, badala yake walitangatanga katika jangwa kwa miaka arobaini. Hizi miaka ya ushusho inapatikana ya kwamba Mungu haku kata tamaa juu yao.Je weweumewahi kujaribiwa kukata tamaa? Juu ya Mungu?Juu ya watu? Juu yako mwenyewe? Kukumbuka upendo wa Mungu na kujitolea kwake kwaekelea wewe haubadiliki. Yeremia aliandika, “ Bwana amenitokea ya kale kwangu,[akisema ]: “Ndiyo, nimekupenda wewe na upendo wangu wa milele; kwa hivyo kwa fadhili nime kuvuta wewe; (Yeremiah 31:3) Huu “upendo wa milele” na fadhili” yote inafunuliwa kikamilifu katika Yesu Kristo,, na inapatikana kwa ajili yako na mimi, na sio kwa sababu ya ustahili wetu, ila ni kwa kustahili kwa Yesu.Hii ni sababu ya kutufanya sisi tusi kate tamaa-Kustahili kwa Yesu kumewekwa kwa akiba yetu. Uhalalisho wa sheria hushindwa mwishowe; neema hushinda.

Na: Peter Youngren

As founder of World Impact Ministries, Celebration Bible College, Way of Peace and the Celebration Churches in Toronto, Hamilton and Niagara, Canada, Peter is committed to equipping believers to fulfill their purpose before the return of Jesus Christ.

Mengi Kuhusu Peter Youngren | Nakala iliyoandikwa na Peter Youngren