Kila baraka iko ndani ya Yesu.

Na: Joseph Prince
Kutoka: August 2009
Wakati Mungu alileta agano jipya la neema. Alimtuma Mwana wake mpendwa Yesu na sio fungo mpya la amri. Kwa hivyo neema ni mtu, na siyo mfunzo. Na kila baraka ambayo tutaweza kuhitaji hasiwezi kutenda na yule bwana Yesu

Ukristo siyo njia ya hesabu fulani. Mungu hakutuangalia sisi, na kutuona katika dhambi zetu na kututupa katika nakala ya maelekezi. La.

Mungu aliupenda ulimwengu jinsi hii kwamba alitupa mtu- Mwana Wake, Yesu Kristo.Bwana akiwa pamoja nanyi nyote mnaye mhitaji maana Bwana Mwenyewe ndiye anaye barika kwa haki, utakatifu, ufanisi, ushindi, kibali, mahitaji, uponyaji, hekima na zaidi sana.

Yesu ndiye Mimi NIKO

1 Wakorintho 1:30
30Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu
na haki na utakaso na ukombozi - Sasa hii ni ajabu! Tambua ya kwamba Mungu hatua hekima ila kwake Yesu. Yeye ndiye hekima yetu! Hatuna utakaso au utakatifu unao hundwa au tengenezwa.Yesu ni utakatifu wetu! Chapa yake ndiye ukombozi wetu!

Mungu hasemi “Nita kupa uponyaji,”au “ Nita wapa ninyi afya.” Yeye anasema, “MIMI ndiye afya yenu! MIMI ni uponyaji wetu!”

Afya, uponyaji, mahitiji na mapato, siye vitu tu au vipawa ambavyo Mungu hutoa. Mungu hukupa wewe Yesu. Yeye ni chote chote unacho hitaji.

Katika Mlima Moriah ambako Mungu alitolea Abrahamu mwana kondo kama dhabihu badala Isaka, tuna ona kutachwa kwa kwanza kwa majina yenye ukuu ya Mungu- Yehovah Yire. (Mwanzo 22:1-14) “ Yire” ina maanisha kuona na kutoa,” lakini kwa Kiebrania ya maanisha Bwana, Yehovah, ni Yire! Kama vile hauwezi kutenganisha msamaha kutokana anaye semehe, haupati ufanisi bila kutoka kwa Yahova. Yeye ndiye toleo lako, ufanisi na mahitaji!

Katika Kutoka 15:26, tuna pata kutachwa kwa jina Yahovah – Rafa, mahala ambako Mungu aliponya maji yao yaliyokuwa chungu yaliyo kuwa huko Marah ili watoto Waisraeli wanywe. Katika Kingereza, hilo jina mara nyingi linatafsiliwa kuwa “ Bwana anaye ponya wewe”, lakini katika Kiebrania, kwa hakika inamaanisha “Mimi ni uponyaji,” au “ nitawapeini nyinyi afya” Yeye anasema, “ MIMI ni afya yenu! MIMI ni uponyoji wenu!”

Samueli wa kwanza 15:29 inasema, “aliye bora kuliko wewe. 29Yeye aliye Utukufu wa Israeli hasemi uongo wala hana kigeugeu,….” Neno “bora kuliko” hapo natsach katika Kiebrania, lina maanisha “ushindi unao dumu”—- ushindi unao endelea. Tambua ushindi ni mtu—Mungu mwenyewe. Hata ushindi ni Bwana! Yeye ndiye Nguvu, ufanisi na ushindi wa watu Wake!

Iwe hali gani maishani mwako, iwe ni kazi gani unayo fanya, bwana kuwa nawe ndiye yote unayo hitaji kutembea nawe au katika hali yako. Ufanisi wako hautegemei mambo yaliyo chini ya mabadiliko. Yote yanategemea yule mtu asiye badili yaani Bwana Yesu, aliye yeye yule jana, leo na hata milele!

Kwa hivyo, unaona kuna kitu kibaya, wakati anataka tu vipawa, lakini hauna moyo kwake yule mtoaji,

Hekima Ina Mikono Miwili, Kwa hivyo Chukua yote!

Watu wengi wanataka hekima. Wengi wana taka kuwa na utajiri na heshima, maisha marefu. Lakini hawaoni yule mtu aliye hekima, na kwamba iko katika wepo wa Bwana anaye kufanya wewe kuwa mwerefu. Wala hawatambui maisha marefu haiwezi kutenganishwa na yule aliye Uzima.Yesu amefanyika kwetu hekima—na ameketi katika mkono wa kulia wa Baba.(Waebra 12:2) Yeye ni hekima ya kweli. Katika Bibilia, hekima imesemekana kuwa na mikono miwili. Katika mkono wakushoto kuna utajiri na heshima, na mkono wa kulia urefu wa masiku.(Methali 3:16) Kwa hivyo katika Kristo Mwenyewe kuna yote katika mkono wa kushoto na kulia ya hekima——utajiri na heshima, na wengi wa masiku!

Katika Kumbukumbu 30:19 Mungu aliwambia wana wa Israeli, Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, Yeye akaongeza.

Kumbukumbu la Torati 30:19-20
19…. Basi chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kusihi; 20…uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa BWANA ndiye uzima wako na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi – Wingi wa siku ni mtu! Bwana ni uzima wa wingi wa siku zako. Yeye ni uzima na weponi mwake Kuna uzima.

Makosa ya Suleimani

Sulemani alikuwa kama miaka 20 amri wakati Bwana alipomtokea katika ndoto na kusema, “ Niulize unayo taka?” Suleimani akasema, “ Bwana nipe hekima.” Na Mungu akajibu, “Lo, nime kupa moyo wenye busara na ufahamu kuliko mfalme mwengine wowote kabla na mbele yako.” (1 Wafalme 3:12) Watu wengi hawatambui ya kwamba Mungu pia alisema haya:

1 Wafalme 3:13-14
13Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima,…..14Nawe kama ukienenda katika njia zangu….. na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.’’

Tambua ya kwamba maisha marefu - wingi wa siku - ilikuwa ni sharti? Mungu alisema, “Ukienenda katika njia zangu, basi nitakupa maisha marefu.”Tunajua hekima ya Suleiman haiku dumu na kwamba miaka ya baadaye alipotoka sana. Ukilinganisha misema yenye busara zilizo nakiliwa katika Muhubiri aliandika vitu kama, “Kwa kuwa hekima nyingi huleta huzuni kubwa, maarifa yanapoongezeka, masikitiko yanaongezeka.” (Mahubiri 1:18) Na akafa kama angali mchanga - hakika karibu amri ya miaka 60. (1 Kings 11:42-43) Nini ilifanyika?

Katika mjibu hii,inatuambia wengi wetu hufa kifo katika umbo na sera kwa sababu hatupalilii wepo wa Bwana.

Suleimani alibadilisha miongu katika miaka zake za badaye. Alisahau ya kwamba Mungu alikuwa hekima yake kweli, ufanisi, na chanzo cha mali. Bila Bwana, Mtoaji, kile kipawa kitakuwa kisicho timiliza na kilicho haribika. Suleimani alikuwa tu na hekima ya kushoto.Hakuwa na mkono wa kulia, sababu Mkono wa kulia wa Mungu ni Bwana Yesu Kristo na Suleimani alikuwa amekata tamaa kwa Bwana.

Kwa hivyo una ona kuna kitu kibaya wakati mwamini anataka vipawa, lakini hataki kuwa na moyo wa yule Mtoaji.

Sio tu jambo la kufikiri, “Yesu ndiye yote ninayo hitaji, sihitajia kazi au fedha.” Ina husu kumfanya Yeye kuwa hitama yako.

Daudi Alijua Chanzo Chake Alikuwa Nina

Sasa Daudi alikuwa mtu anaye pendeza moyo wa Mungu. (Matendo 13:22) Yeye ali dhamini sana wepo wa Bwana.Yeye alikuwa mtu aliye zungumza na Bwana mengi. Yeye alipalilia wepo wa Mungu.Yeye aliweza kuimba jangwani mbele ya kondoo, mahali ambako hukana aliye jua ya kwamba yeye alikuwepo! Katika 1 Samueli 16:1-11, wakati nabii Samueli alikuja kumpaka mafuta mmoja wa wana Yese awe mfalme, Yese alisahau kuhusu Daudi.

Daudi alikuwa uwanjani akiimba, zaburi na sifa na maabudu. “Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema, upendo wake wadumu milele. (Zaburi 118:1) Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai midomo yangu itakuadhimisha…. (Zaburi 63:3)” Alicheza kinubi chake bila msikilizaji ila Mungu. Hii sio mafundisho fulani au dini. Hiyo ni uhusiano wakati! Wakati Daudi alipo kutana na Goliati, licha ya kuwa tu kijana, hakuwa na uwoga maana hakuwa hofu ya jitu, ila hofu ya Mungu.

1 Samueli 17:45-46
45Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki (fumo) lakini mimi ninakujia kwa jina la BWANA Mwenye Nguvu, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana…. 46Siku hii leo BWANA atakutia mkononi mwangu, nami nitakupiga na kukukata kichwa chako. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya jeshi la Wafilisti, nayo dunia yote itajua kuwa yuko Mungu katika Israeli.

Miaka nyingi badaye, wakati alikuwa mfalme, alifanya uasherati na Bethashiba, alifanya dhambi kwake, yule mumewe Uraiah, na watu wake. Lakini wakati Mungu alipo mtuma nabii Nathani kumkabili yeye, Daudi alianguka chini kwa magoti yake na akasema, “Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi…..” (Zaburi 51:4) Alihofu sana yule mtu aliye umia sana alikuwa ni Mungu!

“Usinitupe kutoka mbele zako,” (Zaburi 51:4) ombi alilo fanya. Mungu usiondoe wepo toka kwanngu.Hi ndiyo iliyo nibariki mimi.”

Kile Bwana Anataka Ni Wewe

Leo hii hatuhitaji kuhusika sana vivyo hivyo kama Daudi, maana hatuna hofu ya kwamba Bwana atatuacha sisi. Mungu anatupenda na ametuhaidi ya kwamba hatatuacha au kututupu sisi.( Waebrania 13:5) Lakini wakati mwingine sisi hupuuza mambo.Tuna sahau kupalilia Wepo Wake.Wakati mwingine tuna sahau kusema na Yeye mpaka tunapo fika kanisani Jumapili, karibu ni kama “ Habari, Bwana!”

Unapo mpenda mtu, unamthamini wepo wake. Unatamani.Utaipalilia na kuwajibikia maana kwako ni thamana! Ni kitu kimoja kujua kimasomo ya kwamba Bwana hawachi wala hatupilii wewe, ila kitu kingine ni kupalilia wepo Wake na kumwonyesha ya kwamba Yeye kwamba una amini.

Bwana ana onea wivu kutukuwepo kwako. Ana kupenda wewe. Yeye anataka awe na uhusiano wa kibinafsi na wewe. Yeye haheshimu watu, ila Yeye ni mheshima wa wale wanao mheshimu Yeye na wanao thamani wepo Wake. Na Mungu hatoi viwango vya vidonge na vipande- Yeye Mwenyewe ni uponyaji wako, toleo, na hekima yako. Kwa wingi unapo heshimu wepo Wake, kwa wingi utamwona Yeye akidhirika katika utukufu!

Wakati binti yangu Yessica alikuwa tu mtoto mchanga, twalikuwa na wakati alipo kuwa na homa na alikuwa analia usiku, ninge mwekea mikono mara kadha, nikiomba na kukemea… kila aina njia nilizo jua, lakini bila matoke mazuri. Lakini wakati wowote nilipo acha kutafuta uponyaji, na nikaanza kutafuta mponyanji, mambo yalibadilika! Ilikuwa mpaka wakati mtizamo wangu haukuwa juu ya mtoto wangu na hapo Yesu akawa mkubwa katika dhamira yangu kuliko ugonjwa wake, ndipo matokea mema yakaja.

Tafuta wepo wa Bwana! Yeye ni Yehaovah – Rafa, Yeye mwenyewe ndio uponyaji, na wepo wake unaponya wewe!

Wepo wa Bwana Ni Ufanisi Wako

Na sasa tuangalie hadithi ya Yusufu. Katika Mwanzo 39:2 Bibilia inasema, “BWANA alikuwa pamoja na Yosefu, naye akastawi, Yosefu akaishi nyumbani kwa bwana wake Mmisri.

Iwapo una shangazwa, Yusufu hakuwa katika afisi ya hali ya juu mahala fulani, akiwa na afisi kubwa na kujivalia suti ya vipande tatu. Mwanzo 39:1 ina tuambiaWakati huu Yosefu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri
aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yosefu kutoka kwa Waishimaeli waliomleta Misri.” Tuna angalia kijana aliye mateka! Kijana mateka wa umri wa miaka 17. Akisimama pale katika soko la watumwa, akiwa uchi kugakuliwa, lakini kitu cha kwanza bibilia inasema kumuhusu yeye ni kwamba Bwana alikuwa naye, “na alikuwa mtu aliye faulu.” Je Yusufu alikuwaje aliye faulu?

Mwanzo 39:3
3Potifa alipoona kuwa BWANA alikuwa pamoja na Yosefu na kwamba BWANA alimfanikisha kwa kila kitu alichokifanya, Wow Potifa aliona ya kwamba Bwana alikuwa na Yusufu. Aliona Mungu ali mfanya Yusufu kustawi. Yule bwana alikuwa mtaifa bila karama ya hata ndogo ya umbambanuzi katika mifupa yake, lakini aliona haya!

Potifa aliona udhirisho wa wepo wa Bwana katika maisha ya huyu kijana mtumwa. Mungu hakuwa pale kuwa wa mshika mateka wa kiroho! Nina amini wakati Yusufu alipo panda nyanya, nyanya zake zilikuwa kubwa kuliko za mtu mwingine awaye. Alipo chunga farasi (Wamisiri walitunza farasi), kila farasi ali itikia sauti yake kana kwamba alikuwa kama wanao amrisha farasi. Yule mtumwa mdogo alikuwa na kibali kubwa hata akashika umakini wa mke wa bwana wake!

Nina amini Yusufu alijali sana wepo wa Mungu maana wakati Mke wa Potifa alipo jaribu kutongoza yeye, alikata akisema, “Ni vipi ninaweza kufanya haya na nimtende Mungu wangu dhambi? (Mwanzo 39:7-9) Hakuna aliye kuwa karibu kumsikia akisema ila ni yule mwanamke. Haikuwa kwa kuonyesha. Yusufu alikuwa akisema, “Mungu yupo hapa” Matukio ya baadaye ya Yusufu katika Misiri pia ilithibitisha alimtumainia Bwana kama toleo, hekima na ufanisi wake. Yeye alifurahia kibali na ufanisi wa namna hii kwamba akafanyika wa pili katika utawala!

Je unataka ufanisi wa namna hii? Alafu, usi sahau kile kitu cha kwanza - “ Bwana alikuwa na Yesu.”

Ona Yesu ako Hapa, Hivi Sasa

Bibilia inasema Bwana ndiye msaada uliyopo. (Zaburi 46:1) Alipo fika pale kaburini pa Lazaro, Lazaro alikuwa amekufa tayari siku nne. Maritha aliye kakaye Lazaro, alimwambia Yesu, “Ungekuwepo hapa” ndugu yangu alikuwa mgonjwa, na hangekufa.” Na wakati Yesu alimwambia, “Ndugu yako atafufuka tena,” Aliitikia na kusema, “Ni jua atafufuka tena katika siku mwisho.” (Yohana 11:20-24) Alirudisha Yesu kwa mambo yaliyo pita na yajao, bila kutambua ya kwamba wepo Wake hapo ndilo jawabu!

Yesu alitangazia yeye, “Mimi ndiye ufufuo na uzima!”( Yohana 11:25) Mungu kila wakati ni MIMI niko. Yeye siye nilikuwa au nita kuwa.Tambua ya kwamba katika injili hakuna aliye kufa na au alikaa hivyo mfu katika weponi Mwake?

Upande mwingine hii ina tuambia ya kwamba wengi wetu tuna pitia mauti katika umbo na mifano nyingi maana hatuja palilia wepo wa Bwana.

Hatuja jali sana kwamba Yeye ni msaada wetu uliyopo wakati wa mahitaji.

Kwa hivyo palilia wepo wa Bwana kama vile unge palilia wepo wa rafiki au wa mwanandoa mwanzako, ongea, zungumza, thirisha shukurani zako! Usi jitende kama upo sehemu ya vyombo vya mbao! Fanya macho kuelekea mke wako pale chumbani! Toka pale mlangoni kabla kuondoka kumpuzu yeye. Sema “habari” kwa yule mtenda kazi katika kituo cha mafuta.

Ukitembea mahala palipo na watu wengi, sema kwake Yesu, “Wow, Bwana, ni ya kumfinyanga leo!” Watu, hamwezi kusema, “ Bwana Yesu, huyu ni msichana mzuri!” Juu ya yote uliumba mwanamke, na Yeye ndiye utakatifu! Na hata kama kitu kinaweza kukasirisha, mwambie Yeye! “Bwana mimi si shukuru hili juu huyu mtu.” Angalia kuona upepo wa mbinguni katika mambo madogo, kama vile mtoto anapo geuka na kutabazamia wewe, au unapo weza kupata sehemu kubwa ya kuwegeza magari. Mambo haya sio ya akiajali - Mungu anasema, “Hey, mimi niko na wewe”.

Iwe namna gani, wewe geuza macho yako kuelekea Yesu. Mwabudu Yeye. Kama uwezi kuimba, ongea tu! Bibili ya sema, Mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni”

Pata utulivu Katika Wepo Wake

Mahala popote Bwana yupe na wepo Wake upo, kuna utulivu.

Utulivu ambao hautiishwi chini ya nguvu za angani hali ya nje.

Moses siku alimwambia Mungu, “’ Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua nami nizidi kupata kibali mbele zako.” (Kutoka 33:13) Bwana akajibu.

Kutoka 33:14
14…. “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.’’ Yule aliye nena Musa alikuja katika mwili na akasimama mbele Wayuudi watu wa siku Yake ambao walikuwa na mzigo mzito wa sheria na amri, na akasema,


Mathayo 11:28
28“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Tafsili iliyo tiwa sauti (Amplified) inasema hivi- “Nita kusababisha kutulia, Na katika Kiyunani, kwa fasihi inasema “ nitawatuliza

“Njooni kwangu Mimi”, Yesu anasema. Sio nchi, au mlimani, au dini, ila ni kwake Mwenyewe.

“Njooni kwangi” na wepo Wangu uta sababisha nyinyi kutulia.Katika wepo Wangu kuna utulivu. Mimi ndiye utulivu. Ibilisi hawezi kufanya kazi mahala kuna utulivu—eneo lake ni kuto tulia, usumbuvu na mzongo.

Tunazo baraka ambazo zilizo tulizwa, maana wana tegemea kwake Yesu anaye ishi ndani mwetu. Kwa sababu uponyaji, urefu, ustawi na ufanisi vyote vina tegemea mtu asiye tingizwa, aliye na nguvu zote, anaye jua yote na mwema kwa yote, anaye penda kwa vyovyete, tuna usalama usio weza kuzongezwa! Amani isio nenwa!

Nakala hii imetolewa to kwa ujumbe, Kila Baraka zake zimo katika mtu ambaye ni Yesu, ulio hubiriwa mchungaji Joseph Prince mwezi 7, 2007. Kupata ujumbe wote wa hii nakala, tembelea mtandao on line store at http://www.destined2reign.com

 

 

 

 

Na: Joseph Prince

Joseph Prince is the senior pastor of New Creation Church — a dynamic and fast-growing church in Singapore, which has a congregation of 18,000 members. His ministry as pastor, teacher and international conference speaker focuses on unveiling Jesus and revealing His heart to the people.

Mengi Kuhusu Joseph Prince | Nakala iliyoandikwa na Joseph Prince