Neema ya Mungu – ujumbe unao kuweka huru!

Na: Steve McVey
Kutoka: July 2009
Patikana ndani ya: Injili ya Neema
Nilikuwa nikimwomba kwa ajili ya uamsho kanisani mwetu, lakini tuna hitaji zaidi ya uamsho.Uamsho ni wa ajabu, lakini huja na huenda.Tunahitaji mwondoko toka kwa Mungu uje na kudumu.Tuna hitaji uumbaji mpya kutoka kwa ufunuo, ukileta mapinduzi.

Neema italeta wewe toka nyumba ya jela, toka maisha yaliyo chini ya Sheria na kuleta wewe katika “nyumba ya karamu” ya neema ya Mungu. Mimi nina jiona vema sana baada ya kuwacha dini yangu iliyo kuwa tupu. Nilikuwa mdini kwa miaka nyingi, na nili amini hivyo ndivyo ilipaswa kuwa. Nalifikiri Mkristo alipaswa kuwa na tabia fulani. Lakini maisha ya Kikristo siyo tendo. Inafaa tutulie ndani ya Kristo na turuhusu Yeye aishi maisha Yake kupitia sisi. Ujumbe nitakao shiriki na nyinyi ni rahisi: Kuwa wewe mwenyewe!Jua wewe ni nani ndani ya Yesu Kristo!

Uzima mapya

Katika 2 Wakor 5:17 Bibilia inakuambia ya kwamba wewe ni kikumbe kipya katika Kristo. Wewe yule mtu ulivyo kuwa. Mungu alichukuwa yule mtu ulivyo kuwa na akafa msalabani. Basi akakupa wewe maisha mapya - Uzima wake mwenyewe.Uzima wenye haki. Uzima mtakatifu. Uzima usio wa kawaida.Uzima ulio kuleta katika ushirika na wa pamoja na Yule Baba kupitia Mwana Wake, Yesu Kristo.

Huu ujumbe wa neema ni rahisi. Una sema: “Wacha kujaribu na anza kuamini!”

Na sasa usi jaribu kujitenda kama mtakatifu tena. Ni bure kujaribu kujifanya mtakatifu. Ni vibaya sana hata kuwa karibu na wengine wanajaribu kuwa watakatifu. Katika kuonekana, nao wanajua sawasawa inayo wapaswa kufanya kuwa zaidi ya wao.Ujumbe wa neema ni rahisi. Unasema: “ Wacha kujaribu na anza kuamini!” Koma kutenda kazi katika tamaa ya dini ili kuendelea mambo ya rohoni na wewe kuja na utulie katika Kristo! Koma kutumia nguvu zako ukijaribu kufikia baraka za Mungu!

Naliweza kufikiri kutumia nguvu zangu ilikuwa ni jambo kuu. Lakini Mungu hakutaka sisi kutumia nguvu zetu, ametuita kuendelea kutumika tunapo kuwa tume tulia. Epu ni kukumbushe wewe, huu sio ujumbe, mimi ni mjumbe tu. Ujumbe unatoka kwa Bwana Yesu mwenyewe! Ni Yesu aliye sema: “Njooni kwangu, ninyi nyote sumbukana na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwamaana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.’’

Je unaweza kuona uzima Yesu ametoa? Anatumia maneno kama mwepesi na pumzika Yesu anasema: Njooni kwangu na mpate pumziko!” Dini inasema: “Fanya kazi!” Yesu anasema: Nira yangu ni laini, mzigo wangu ni mwepesi!” Dini inasema lazima ufanya kazi kwa ajili Yake. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya dini na maisha ya Kikristo. Maisha ya Kikristo ni uhusiano wa kibinafsi na Mungu kupitia Yesu Kristo.

Sheria ya dhambi na mauti

Warumi 8:2 inasema: “ Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.”

Bibilia ina eleeza ya kwamba kuna sheria mbili tofauti zinazo fanya kazi katika hii dunia na mojawapo ni sheria ya dhambi na mauti.Ni sheria ya ulimwengu wote ambayo inafanya kazi katika njia moja kotekote kwa wakati moja. Kama sheria ya kuruka na kuanguka inaweza angusha kitu kuelekea kati mwa nchi, sheria ya dhambi na mauti ita jaribu kuvuta watu chini na katika dhambi.

Ni vipi tutashinda hii sheria kama Wakristo? Nina badhi ya habari mbaya kwa ajili na tena nina habari njema. Habari mbaya ni kwamba hauta wahi pata ushindi kupitia nguvu zako mwenyewe. Haijalishi ni jinsi gani umejitolea na kwa muda gani utajaribu, hautaweza kuishi maisha ya Kikristo kwa viwango vya Mungu. Unahitajika hata hiyo utupilie mbali! Habari njema ni kwamba Yesu anaweza na anaweza kuishi maisha haya kupitia wewe.Wewe hauzi - lakini Yesu anaweza!

Inakuwa mzururo wa maisha;jiweke wakfu, jaribu, shindwa,jiweke wakifu, jaribu,shindwa…

Kwa miaka 29 nili endelea kuota maisha yangu kwa Mungu. Kila wakati nili haidi kupigana kwa nguvu ili nimwiishie Yeye. Ni jitoa tena mimi tena na tena. Nilijaribu kwa nguvu, lakini nilishindwa! Ikawa ni mzururo wa maisha; jitolee tena, jaribu, shindwa, jitolee tena, jaribu, shindwa…. Kwa miaka 29 niliendele kufanya hivyo! Mwishowe nili elewa ya kwamba haingefanya kazi. Unaweza kusema nilikuwa mimi ni kujifunza polepole. Nili fanya jambo hilo kwa miaka 29 na hainge fanya kaz!

Je ni mara ngapi umejitoa wakfu wewe mwenyewe kwake Bwana? Nina habari njema kwako! Unaweza kukoma tokea hapo, maana haiwezi kufanya kazi!Wewe unasema: “Lakini ninafikiri itafanya kazi” Na sasa kwa nini uyafanye ukirudia rudia? Unajua haitatenda kazi! Hatuja itwa kujiweka wakfu sisi wenyewe kwake Kristo. Tunapo fanya hivyo,tuna ng’ang’ana katika nguvu zetu wenyewe kuishi kwa ajili Yake. Shida hapo ni sisi wenyewe. Shida sio kujiweka wakfu sisi wenyewe tena mara ingine, ila ni kukoma kung’ang’ana katika nguvu zetu wenyewe.

Sheria Mpya yenye nguvu

Umetambuwa hauta ishi maisha makamilifu kwa ajili ya Yesu katika uweza wako mwenyewe. Tunaweza kuwacha kuomba: “Bwana, nipe nguvu.” Badala yake, tunaweza kuomba: “Bwana, mimi ni mdhaifu na kila wakati mimi nita kuwa mdhaifu ndani yangu. ila wewe ni nguvu!” Ni katika udhaifu wa wetu wa kibinadamu ambako nguvu za Mungu zina onekana. Sheria ya dhambi na mauti ita kukokota chini. Unaweza kuwa na imani yote na kujitolea kwote ambako unafikiri unahitaji kushindwa, walakini hautawahi kufaulu. Nina weza kupanda juu ya dari la jingo mrefu, ukiamini kwa dhati ya kwamba unaweza kupaa. Nina weza ruka toka kwa paa, niki punga mikono zangu kwa imani yote mwanadamu anaweza kuzaliwa, lakini nimehakishiwa wa kuanguka chini.

Bibilia inatuambia kuhusu sheria ingine,ni sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu. Iwapo mtu anaweza kupanda juu ya jingo mrefu akiwa na banda la ndege, utajua hata anguka kama yule mtu anaye punga mikono zake. Lile banda la ndege inaleta utofauti mwingi kwa huyu bwana, maana inaleta katika mchezo huu sheria mpya - sheria ya kupaa kwa ndege. Hiyo sheria ni kuu sana kuliko sheria ya kuruka na kuunguka. Sasa huyu bwana anaweza kutulia chini ya banda la ndege na kushinda sheria ya palipo na uzito.

Yesu anasema: “Njooni kwangu na mpate pumziko!” Dini inasema: “ Fanya kazi!”

Sheria ya dhambi na mauti itatukokota sisi chini, lakini tunapo tulia katika imani kwamba Kristo inaishi ndaini yetu - kwamba Yeye anaweza kufanya - hapo basi tunapata ushindi juu ya sheria na mauti. Hauna ushindi katika nguvu zako mwenyewe; Yesu Kristo ni ushindi wako! Unapo tulia ndani Yake na kuruhusu yeye aishi ndani yako, Ata hakisha utembea katika ushindi juu ya ya sheria ya dhambi na mauti.

Kuzulubishwa na Kristo

Hatuna ushindi katika nguvu na uweza wetu wenyewe, ila ni katika Roho wa Mungu. Iwapo unataka kushinda nguvu za uharibifu za dhambi, unahitaji kuja na kutulia katika sheria ya Roho wa Kristo Yesu. Bibilia inasema sisi tume kufa kutenda dhambi. Hiyo haimaanisha hauta wahi jaribiwa na dhambi,lakini kwa uhakika unachukia dhambi kwa sababu wewe umekufa katika kutenda dhambi.

Fikiria bwana ambayo anameza dawa nyingi za kulevya na anakufa. Anapo lala pale makaburini katika jeneza, mmoja wapo wa marafiki zake walio tumia dawa anakuja pale kaburini. Yule rafiki ana inama pale na jeneza na anaseme : “Hei, nina dawa za kulevya hapa! Je unataka hizi vitembe?” Je unajua lile yule bwana katika jeneza atafanya? Hakuna kitu! Yeye amekufa! Mtu aliye kufa ahitaji dawa za kulevya!

Bibilia inasema wewe umekufa katika kutenda. Wewe ulikufa msalabani pamoja na Yesu.

Nimesulibiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Paulo alituambia tujiangaliye sisi kuwa wafu katika kutenda dhambi, lakini tuwe hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Sisi tumekufa katika kutenda dhambi. Wakati dhambi zinapo kuja zikibisha mlongoni mwetu, tunaweza kuthibisha ya kwamba sisi tumekufa hatuwezi kutenda dhambi. Hauhitaji tena kusema la kwa majaribio kwa sababu ya kuwa na jugumu; sasa unaweza kusema la maana HAUTAKI kutenda dhambi! Wewe uko huru! Kwa hivyo kwa nini urudi katika uchafu? Tunao uzima wa Yesu Kristo ndani mwetu na tupo huru.

Wewe weka macho yako kwenye suluhu

Wakristo wengi wemefungwa na sheri.Wao wanajaribu kupigana na majaribio kwa nguvu za wasia wao. Tuna hitaji kujua hali yetu - kwamba sisi tume kufa katika kutenda dhambi. Tena tunahitaji kujua nafasi yetu katika Kristo. Sisi ni pamoja na Yeye sasa. Sisi tume fufuliwa toka mautini pamoja na Yeye. Bibilia inasema iwapo tume fufuliwa na Kristo, tunahitaji kutafuta vitu vilivyo juu, sio vitu vilivyoko duniani.Maana mmekufa, na uzima wenu umeficha katika Kristo ndani ya Mungu.

Mara nyingi kwa umbali, Wakristo wanajaribu kutenda kazi katika sheria ya dhambi na mauti. Wanajaribu kuwa na ushindi juu dhambi kupitia uweza wao wenyewe. Wao huangalia sana dhambi na hujaribu nguvu zao wenyewe kushinda majaribio. Wao hutizama sana dhambi mpaka zimejaa niani mwao. Hauna ushindi juu ya dhambi kwa kutizama dhambi, ila ni kwa kutizama macho yako kwake Yesu!

Nili sikia mtu fulani akifundisha ya kwamba dhambi maishani mwako ni kama magugu katika bustani. Alisema ya kwamba unahitaji kuweka bidii katika kuyang’oa moja baada ya ingine. Lakini kuna shida na thelojia hii, na ni kwamba magugu hukuwa upesi sana.Ni napo kuwa nina fanya kazi na kung’ang’ana kutoa magugu mahala moja, yangali yana endelea kukuwa katika maeneo mengine. Ni msururo mmbaya wa milele.

Wewe hauna ushindi juu ya dhambi kwa kuangalia magugu.Una shinda kwa kuangalia kwake Yesu! Tunapo angalia Yesu, nguvu za dhambi zita kwisha na kupotea. Dhambi sio suluhu - Yesu ndiye suluhu! Yeye Ni ushindi wetu juu ya dhambi. Unapata ushindi kwa kuangalia macho yako kwake Yeye!

1 Wakor 15:57 Lakini ashukuriwe Mungu, Yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Waru 8:37 Lakini katika mambo haya yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda.

Jua nafasi yako katika Kristo

Tunahitaji kujua hali yetu. Sisi tume kufa kwa kutenda dhambi! Tunahitaji kujua nafasi yetu. Sisi ni moja na Kristo Yesu!

Tume wekwa huru na uzima wa Yesu! Tumefanyika haki katika kiini cha kuwa kwetu. Roho yetu imekuwa kamilifu kupitia Yesu Kristo. Nafsi yetu imefanyika upya kila siku tunapo tembea pamoja na Yeye. Siku moja, tutapokea mwili ambao ume tukuka na tutukuwa huru kabisa kutoka wepo wa dhambi. Mpaka hiyo siku, tutatulia ndani mwake Kristo Yesu. Hatuishi na kukiri ya kwamba sisi ni wenye dhambi, ila sisi tu watakatifu ambao wakati mwingine hutenda dhambi.Lakini sisi sio wenye dhambi!

Yeye alimzidishia mwana wake na wema wote hata na upendo.

Jinsi unapo jitenda kwa tabia na jinsi ulivyo au haiwezi kuingiana wakati mwingine. Licha ya haya tunaweza kutenda vitu visivyo ingiana na jinsi sisi tulivyo akina nani katika Yesu, hiyo bado haibadilishi sisi katika Yeye. Nina weza kujitenda kinyume na jinsi nilivyo, na bado haibadilishi miye ni nani. Ninge jivika siku moja kama mwanamke, nijivike nguo ya kike na kujipotoa, lakini hiyo haiwezi kunifanya mimi kuwa mwanamke. Katika njia hiyo hiyo, tunaweza kushindwa na hata kutenda dhambi, lakini haibadilishi ukweli sisi ni nani katika Kristo Yesu. Unapo tenda dhambi na kufanya mbaya, haibadilishi wewe ni nani. Unaweza kutenda katika ujinga, lakini ungali wewe ni mtoto wa Mungu.

Upendo usio na Masharti

Mungu ana kupenda bila masharti kila wakati. Wengine wanaweza kuamini Mungu anapenda tu kazi na hufanya kazi chini ya masharti fulani. Wakati mwana mpotevu alitaka kurudi nyumbani mwa baba yake, alifikiri angerudi kama mtumwa katika shamba la Baba yake. Ange ambia baba yake ya kwamba yeye hastahili tena kuitwa mwana wake, ila ange mtumikia yeye. Hii ni kukiri kuliko wazi kwa Mkristo aliye chini ua Sheria: “ Baba nime tenda dhambi! Sistahili tena kuitwa mtoto wako, ila iwapo unaweza kunisemehe tena, nita kutumikia sana na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili yako.”

Wakati mvulana huyu alipo fika karibu na shamba, babaye akamwona yeye alipo kuwa angali mbali sana na babaye akaja akikimbia kumsalamia! Alifurahi kumpata mwanawe kurudi na kampuzu yeye. Mwana hakutoa habari yake. Babaye hakusumbukana kama kichana alitaka afanye kazi kwa bidii - yeye alifurahi tu kumpata mwana wake kurejea nyumbani. Yeye akamrisha watumishi wake kufanya karamu kwa ajili ya mwana wake na kusherekea! Yeye alimzidishia mwana wake kwa wema na upendo.

Iwapo umetenda dhambi basi kimbia urudi mikononi mwa Baba. Hauhitaji kuja ukiwa na ahadi nyingi ambazo hauta timiliza. Kuja kwa baba jinsi ulivyo. Unaweza kufikiri amekugeukia moyo Wake kinyume na wewe, lakini utakundua ya kwamba upendo wake kwa ajili yako hauta badilika.

Yeye hatupendi akitegemea iwapo tuna tenda dhambi au hapana.Yeye anatupendi kwa sharti moja tu: sisi ni watoto.

Yule mwana mkubwa katika methali ya mwana mpotevu hakuwa na furaha juu ya yaliyo kuwa yakitendeka. Yeye alilalama jinsi kwa uaminifu alikuwa ametumikia babaye kwa miaka, lakini babaye hakuwa amemfanyia karamu kama aliyo kuwa akimwandalia mwana mdogo. Kwa ukweli, huyu ndugu alikuwa na baadhi ya kutoelewa kuhusu babaye kama mwana mdogo. Yeye aliamini uhusiano kati yao ulikuwa kuhusu utendaji wa kazi. Mungu anatupenda, sio jinsi tunavyo mtumikia au hatutumikii Yeye. Yeye anatupendi haitegemei iwapo tuna dhambi au hapana. Yeye anatupenda katika sharti moja: Sisi tu watoto Wake.

Wengine wanasema kuhubiri ujumbe wa neema utasababisha watu kutenda dhambi zaidi. Bibilia inasema neema itatufundisha kukana utaua na vita vya ulimwengu. Unapo jua ni kiasi gani Yesu na Baba wanakupenda wewe, wewe uta tiwa nguvu kuishi kwa sheria iliyo juu, sheria wa Roho wa uzima katika Kristo Yesu. Ruhusu Mungu akupe uweza kutembea katika nguvu zake na kujitenda sawasawa jinsi ulivyo katika Kristo.

(Ime chapishwa na kibali kutoka Steve McVey, Rais, wa Grace Walk Ministries , http://www.gracewalk.org -1-813-234-9546”)

 

 

 

 

 

 

 

 

Na: Steve McVey

Dr. Steve McVey is a dynamic author and speaker who inspires Christians to develop a deeper, more intimate relationship with God.

Mengi Kuhusu Steve McVey | Nakala iliyoandikwa na Steve McVey