Neema Huenea Katika Eneo lilo Huru Katika Maisha yako

Na: Joseph Prince
Kutoka: March 2009
Patikana ndani ya: Grace and Faith
Mungu kwa uaminifu huleta Neema Yake katika maeneo yote ya maisha yetu . Neema Yake ina tiririka kwa uhuru… mpaka tutakapo zua mtiririko kwa kuruhusu ibilisi kutufanya kuwa na wasiwasi nakusumbukana!

Katiku usiku huu Bwana Yesu alisalitiwa, katika usiku huu alipo ingia katika shauku Lake na kuteseka kwa ajili yetu Aliwaambia wanafunzi wake:

Yohana 14:27
Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Wasia wa Yesu na ulio kama kipawa kikuu, ni Alitaka awache nyuma kwa wanafunzi Wake kabla kusulubishwa Kwake ni karama ya Amani.

Bwana wetu anaitwa Mfalme wa Salem (Waebrania 7:2) “Salem” yamaanisha “Amani.” Pia anaitwa Mfalme wa Amani.Alipo kuwa hapa duniani, alitembea katika amani hii kwamba Alikuwa katika ushukani. Walijaribu kimpiga Yeye kwa mawe mara moja, lakini alitembea tu katika ya watu hao bila majeruhi (Yohana 8:59). Hakuna ambaye ange mgusa Yeye. Yeye alikuwa na amani yote iliyo kamilifu.

Ibilisi ilipiga tufani katika bahari la Galilaya, lakini aliendelea kula katika mashua. Uvamizi wa Ibilisi haunge mwamsha Yeye toka uzingizini, ila ni kilio cha wanafunzi Wake kilichomwamsha (Mariko 4:35-41). Hata katika mauti yake, Alikuwa katika ushukani. Hakuna aliye chukua uhai wake toka Kwake. Ali toa uhai Wake (Yohana 10:17-18). Alifanya chukuo katika bustani kutoa uhai Wake kwa ajili yetu.

Yule aliye Shalom (Amani) ya God

Yesu alikuwa na sasa yupo katika ushukani kikamilifu .Na sababu mojawapo ya kuwa mwenye nguvu ni kwamba alitembea katika ile shalom (amani) ya Mungu. Neno “amani” katika Yohana 14:27 ndilo neno “shalom” katika Kiebrania. Imaanisha wema, mkamilifu, kukamilika, na pai amani ya Moyo na akili. Kwa kuwa na shalom inamaanisha kuwa na kila sehemu yako — roho, nafsi na mwili — sawasawa.

Sasa Yesu alimaanisha nini alipo sema, “Shalom iwe pamoja nanyi. Sio shalom ya ulimwengu, ila shalom yangu”? Hivi ndivyo alimaanisha: “ Ile shalom mwali ona mimi nikiishi ndani: ile shalom mwali ona mimi nikilala ndani, katika merikebu: ile shalom mwali ona mimi nikitembea katikati mwa watu waliotaka kunipiga kwa mawe: ile shalom inayo fanya Shetani anakosa nguvu ya kugusa Mimi; hii shalom, shaloma yangu niniwapa.”

Hii ndiyo amani Yesu alitupa kwetu sisi. Na sio amani ya ulimwengu inayo kuja kupitia miziki uvumao, utafaghari, au kupumua kwa ndani. Hii ni ya nguvu kushindi hiyo! Hai tegemei hali na inatembea katika mwa dhoruba yamaisha.

Linda moyo wako kuliko Vyote ulinavyo

“Lakini Mchungaji Prince, iwapo Yesu amenipa hii amani, na kwanini ningali ninasumbuka na nina wasi wasi juu ya mambo mengi?”

Ni kwa sababu umeruhusu moyo wako kusumbukana. Tambua tu hapo baada ya Yesu kusema, “Amani nina wapa, amani Yangu nina wapa… ” Alisema,
msi fadhaike mioyoni mwenu, wala msi ogope.”
Wewe msifadhaike mioyoni mwenu wala msiogope. Bwana hawezi “msi” kwa ajili yako. Mke wako hawezi “ msi “ kwa ajili yako. Mimi siwezi “msi” kwa ajili yako. Yafaa “usi”wewe mwenyewe.

Watu wengi wanalinda fedha, kazi, watoto, afya zao na mengine mengi. Lakini Bwana hataki sisi kulinda hizi vitu. Badala yake anataka tulinde mioyo zetu:

Mithali 4:24, Ya NIV
Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindavyo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Lazima tulinde mioyo zetu, zaidi ya yote. Iwapo tutalinda ya hicho kilicho ndani (Yeye hawezi kutulindiya hiyo), Mungu atalinda vitu vinginevyo vilivyoko inje. Iwapo hatuta ruhusu mioyo kusumbukana au kuwa na uoga, haki, amani na furaha ndani ya roho mtakatifu itaanza kumiminika moyoni mwetu, hii kwa kweli ni kutafuta ufalme Mungu kwanza na mambo haya yote ya inje tunayo hitaji yata zidishwa kwetu! (Mathayo 6:33)

Hii yafaa ituletea pumziko. Hatuitahiji kusumbukia mambo mengi. Tunahitaji tuu kulinda mioyo yetu. Watu hufanya maumzi ya kiujinga wakati mioyo yao imesumbuliwa. Wao hufanya vitu ambavyo hawange fanya. Kwa hivyo Linda moyo wako. Bwana aliniambia wakati moja ya kwamba iwapo tunaweza kulinda mioyo zetu kwa kutosumbukana au kuwa oga, basi iwapo ni muujiza tuna hitaji, tutapata!

Njia ya kulinda moyo wako pasipo masumbufu na hofu ni kunuku Yohana 14:27. Wakati wowote shida inapo kuja moyoni mwako au unapo ona hofu, sema “Msifadhaike na wala msi sumbukane.” Na hapo uta achilia uweza wa utimilizo wa maandiko. Na amani ya Mungu itaanza kutiririka moyoni mwako.

Neema Yake katika Bora

Sisi sote tuna maeneo ya udhaifu na nguvu.Kinacho nisumbua sio kinacho sumbua wewe na ni kinyume kwako. Ibilisi anajua ni kiponyezo kipii ata ponyeza kwa kila moja wetu.

Kwa mfano, wakati mwingine naweza kuwa na wasiwasi kwa sababu ninampenda binti wangu zaidi. Sina wasiwasi kuhusu mambo ya fedha. Hata wakati nilipo kuwa mwanafunzi na jamii haikuwa na mapato sana. Mimi sikuwa na wasiwasi kuhusu pesa. Mungu alinipa neema toka hapa nilipo zaliwa mara ya pili yaani kuto sumbukana kuhusu pesa.

Ibilisi hawesi kupata katika maeneo ya maisha ambako hauyajali sana.

Kwa hakika, Bwana aliniambia hivi majuzi, “Mwanangu, je umetambua Ibilisi hawezi kupata katika maeneo ya maisha usio ya jali sana? Maeneo ambayo hausumbukani nayo, hayo ndiyo unaona Neema yangu kwa ubora wake, Mibaraka zangu katika utajiri.”

Alipo sema hayo, nalianza kutumbua kuna maeneo mengine kando na fedha ambako si kusumbukana nayo na ambako neema ya Mungu ili miminika kwa uhuru.

Watu wengine hufikiri ya kwamba shida zao ni ndogo sana kwa Mungu kushughulikia. “Nina aibika kuambia Mungu kinacho nisumbua mimi. Ni kama uvimbe ambao umekuwepo kwa majuma machache.” Sikiza iwapo inasababisha moyo wako kusumbukana, sio jambo ndogo! Mungu anataka wewe umpe Yeye hilo jambo ndogo. Yeye hataki Moyo wako moyo kusumbukana na chochote, kiwe kikubwa au ndogo. Na iwapo uta mpe Yeye, basi usifadhaike moyoni mwako, neema yake ita tiririka kwa urahisi katika hilo eneo la maisha yako.

Roho ana tufundisha Sisi Kuhusu Urefu wa Wimbi La Amani

Kitu kingine nacho taka utambuwe ni kwamba kabla Yesu aanze kuzungumza kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wake, Yeye anazungmza kuhusu mwongozo wa Roho Mtakatifu

Yohana 14:26-27
Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina Langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Amani nawaachia, amani yangu nawapa…

Yesu anatuambia sisi ya kwamba Roho Mtakatifu anatufundisha mambo yote katika urefu wa wimbi la amani. Katika maneno mengine, iwapo unaweza kulinda moyo wako kutokana na kusumbukana kwa shida, iwapo unaweza kukata kuwa na wasiwasi kuihusu na ukaa tu katika Amani, Roho Mtakatifu ataku “kufundisha mambo yote.” Atawaonyesha njia ya kutoka katika hiyo hali!

Ujuzi Wangu Katika Utungu wa Tumbo Kuuma

Miaka nyingi zilizo pita, nalipata utungu katika tumbo langu, na mwishowe nalimwendea Daktari. Akanishawishi ya kwamba nalihitaji kupimwa kwa mashine ya miali ipigayo picha ya tumbo, “Hauwezi ukajua dalili ulizo nazo, unaweza kufikiri si kitu, lakini…” Nili mwangalia Yeye na unajua imani huja kwa kusikia, na pia hofu huja kwa kusikia!

Baada ya mashauri haya, nili jiambia, “Nah sahau yale yote amesema. Miye ni mtu wa Imani!” Lakini haya maneno yaliendelea kunirudia mimi. Na mradi dalili zilikuwepo na hiyo picha haikuwa imechukuliwa, naliendelea kujali sana hizo dalili. Mwishowe nikaenda kupigwa picha ya tumbo. “Kwa nini nisitulie mara moja na kwa yote?” Naliji ambia.

Matokeo ya picha, ikaonyesha kwamba hakukuwa na shida yoyote na tumbo langu. Utungu ulikuwa tu ni dalili za uwongo! Lakini je unajua kilicho tendeka mwezi hizo? Nilikuwa mwangalifu kwa vyakula nilivyo kula. Nalikuwa na hofu kwa afya yangu mara ya kwanza, kiasi kwamba nili anza kula vyakula vya viwanda na hata kunywa mjuzi wa wa Karoti kila siku! Nali mwambia mke wangu, Wendy, kwamba yafaa nile wali nyekundu – na sio wali nyeupe. Kila wakati tulipo kula ilinipasa kuwa na wali nyekundu! Nilikuwa hivyo kwa bidii. Pia nika anza kusoma vitabu vya Kikristo kuhusu vyakula bora. Nika fanya mazoezi ya kupiga mbio kila siku kwa dakika 45 mpaka nilipo konda!

Bado, nikiwa na vyakula vya kiwanda, mjuzi wa karoti na mazoezi ya kila siku, nalienda kumwona daktari zaidi kwa mwezi hizi kuliko miaka wakati siku kula vema wala kufanya mazoezi! Na ilikuwa kwa ajali ya sababu zingine, sio kwa a jili ya tumbu.

Utandaji Wa Ibilisi

Sasa, tunapo angalia nyuma, tunaweza kuona jinsi Bwana alisema ni kweli kabisa. Nilipo anza kuwa na wasi wasi kuhusu eneo fulani katika maishani mwangu, shida zikaanza kuingia katika hilo eneo.

Nilipo kuwa nikitafaghari kuhusu hayo, Bwana akaanza kunionyesha mimi mbinu za utandaji wa Ibilisi, jinsi anavyo tenda kazi. Kwanza, huja kwako na anaona eneo maishani mwako ili akushambuliye. Lakini anajua ya kwamba hana uweza wa kuumiza wewe—- Yesu alimvua uweza wake (Wakolosai 2:15). Kwa hivyo jambo la peke analo weza kufanya ni kupa wasi wasi.

Je unakumbuka yale 1 Petero 5:8 inasema? “Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu Ibilisi, kama simba angurumaye huzungukazunguka akitafuta mtu ili apate
kummeza.”
Mstari unao tangulia ni upi ? “…Mtwikeni Yeye fadhaa zenu zote kwa maana
hujishughulisha sana na mambo yenu.”
(1 Petero 5:7)

Ibilisi hamwezi Mkristo aliye na amani!

Katika maneno mengine, wakati wowote unapo kuwa na fadhaa nyingi na hamtwiki Bwana hizi fadhaa, unakuwa “anayeweza kumezwa” na ibilisi. Lakini iliyo kinyume pia ni kweli: Ibilisi hamwezi Mkristo aliye na amani! La, ni lazima akusumbuwe na, kufadhaisha, akupe wasiwasi na kuogopesha kabla hacha kugusa wewe.

Wasi wasi Inazuia Mtiririko Wa Neema

Hapa kuna mfano ambao Bwana alinipa ili nikusaidia kuelewa yale nina sema .Fikiria kuni mapomba mengi yanayo toka juu mbinguni. Haya mapomba ni yaliyo mapesi na yote yana hudumu neema kuu ya Mungu katika maeneo yote ya maisha yako. Kuna neema ya uponyaji inayo tiririka katika maisha yako, neema ya ustawi, neema ya ndoa na kuendelea.

Mara tu unapo kuwa mwamini, una kuwa mwenye haki kwa imani na una weza “ kupenye kwa imani hadi neema hii ambayo twa simama juu yake.” (Warumi 5:2) Inapo kuja kwa faida na mibaraka za Mungu, sisi sote, tuwe wachungaji au watenda kazi, tuna furahia urithi ule ule. Na sisi sote tupo katika msimamo mmoja katika eneo la neema.

Wakati Yesu alipo kufa msalabani, twalikuwa na tetemeko la Ardhi na moyo wa Mungu ukawa wazi, na mito za upendo Wake, neema, rehema na mibaraka zika jitokeza. Na kwa sababu Mungu ni wa milele, mito hizi ni za milele. Zimekuwa zikitiririka tangu Yesu afe. Zina tiririka kila wakati.

Lakini linalo tendeka ni kwamba tunapo weza kuwa na wasiwasi, ina kuwa ni kama tuna shikilia mfereji ambayo ni nyepesi, na tuna zuia mtiririko wa neema ya Mungu katika maeneo hayo maishani mwetu, Kwa wingi tunapo kuwa na wasiwasi, kwa wingi ndipo kwa nguvu tuna shika pomba hili sana na ndipo zaidi lina fungana. Je neema Yake ingali ina tujia toka mbinguni? Ndiyo, lakini mfereji ume zibwa na wasiwasi yetu na shughului zetu. Upande mwingine katika maeneo hatuja kuwa na wasi wasi, neema Yake hutirika kwa uhuru, ikizalisha, fungu la thelathini, sitini na mwishowe matokeo ya mamia.

Sasa unapo shutuliwa, kufadhaika, wasiwasi na kuogopa kuhusu eneo fulani maishani mwako, sema kama mambo ya fedha, hapo unampa ibilisi upenyezi katika eneo hilo. Ibilisi hana uweza wa kukomesha neema inayotiririka katika fedha zako. Hawezi kushika huu mfereji. Mungu hawezi ruhusu hiyo. Mtu wa kipekee anayeweza kushikilia ni wewe.

Dalili za Udanganiyifu Za Kufanya Wewe Ufadhaike

Kwa sababu ibilisi anajua ya kwamba hana uweza juu yako, atakacho fanya ni kupa wewe dalili za uwongo kukufanya wewe uwe na wasiwasi. Sema kama afya yako, kwa mfano. Ibilisi hawezi kukuwekea tu magonjwa. Hana haki ya kufanya hivyo kwa mtoto wa Mungu kwa sababu Yesu amechukuwa dhambi zenu msalabani .Amechukua adhabu yenu na kubeba magonjwa na uchungu wenu. Kwa mapigo yake mmeponywa (Isaiah 53:4-5). Hauwezi pia kulaniwa kwa laana yoyote kwa sababu Kristo ame amewakombowa kutokana na laana ya Sheria (Wagalatia 3:13).

Yote ibilisi anaweza kufanya ni kukupa wewe dalili zindanganyazo na kutumaini ya kwamba uta weza kufadhaika. Mara unapo fadhaika na kuwa na wasi wasi kuhusu hizo dalili na kuanza kufikiri ju yake kila wakati, uta anza kuzuia mtembeo wa neema ya Mungu katika afya yako. Tena Mungu angali ana leta neema. Yeye ni mwaminifu. Ni wasi wasi yako inayo fungu mfereji.

Ilete Kwa Bwana Katika Maombi

Kwa hivyo kata kuwa na wasiwasi. Usi fadhaike moyoni, wala usi jiruhusu kuwa na hofu. Wakati una kitu ambacho unahusika nacho, wewe kilete kwake Bwana katika maombi.

Wafilipi 4:6-7
Msijisumbue kwa jambo lo lote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itawalinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Usiwe na mashaka. Hakuna kutumia faida katika kuomba maombi ya wasi wasi. Wewe mwambie Bwana kuhusu hiyo shida na mtwikeni fadhaa zenu zote maana Yeye hujishughulisha na maombi yenu. Wachilia iende. Na mshukuru bwana ame wasikia na una shughulikia kila kitu kuhusu hilo jambo. Ukifanya hivi kata kufadhaika, “ amani ya Mungu inayo pita ufahamu wote, ita Linda moyo na nia yako kupitia Kristo Yesu.” Kumbuka: Ibilisi hawezi kukabila Mkristo aliye na amani.

Baba Ana Tutaka Tuwe Watu Wasio Jisumbua


Wakati binti wangu Jessica, alipo ananza masomo ya mzingi, yaani 1, angeli mkosa mama yake na kupiga simu nyumbani wakati wa mapomziko. Siku moja, hangeweza kumpata mamake na akaingiwa na wasi wasi, ilikuwa ni jambo la kutisha kwake.

Alipo rudi nyambani siku hiyo, nali mzungumzia kuhusu yaliyo tokea. Na nali jishughulisha na yeye sana. Ili nihumiza kumwona yeye kama ame fadhaika. Aliendelea kusema, “Sitaki kuenda shuleni. Ni kama ndoto ya uta. Nini taka kuwa na Mama.“ Nilijaribu kushindana na yeye, lakini ilikuwa ni kama yeye hata hanisikii mimi.

Hitamaye nika mwacha na mama yake na nikaenda kawa chumba changu. Nali weza kusumbukana binti yangu alikuwa na wasi wasi katika umri mdogo kama huu. Nilikuwa nina ona hasira kidogo kuelekea yeye. Kwa hivyo nikakaa chini na kuambia Bwana, “Bwana, sitaki yeye asumbuliwe. Angali mdogo sana. Nami ninaona mbaya kumwonea hasira yeye. Mimi nime changanyikiwa, Bwana.”

Bwana akaniambia mimi, “Mwanangu mbone una husika sana na yeye?”

Ni kasema, “Sawa, sitaki yeye asumbuliwa.”

“Je hiyo ndiyo sababu halisi?”

“Ndiyo.”

Twalikuwa na unyamavu kwa muda kidogo. Alafu. Akaniuliza. “Ni sababu gani inayo kufanya wewe hautaki yeye asi sumbukane?”

Nili fikiri kwa muda kidogo na kama umeme nikaona ile sababu yake halisi: Nina mpenda Jesisca wangu sana , kwamba nina mtaka yeye asijali! Nina taka yeye afurahie maisha. Sitaki yeye, katika umri mdogo kama huu, awe akifikiri, “Itakuweche iwapo nikipiga simu na Mama asikuwepo huko? Ita kuwaje… Itakuwaje… ”Sitaki yeye awe na wasi wasi kwa sababu nina mpenda sana.

Ina nipendeza sana ninapo msikia akianguka kicheko anapokuwa ana tizama kipindi akipendacho katika runinga, au Wendy na mimi tunapo pusu tumbo lake pale kitandani, inatufanya kuwa na furaha kusikia yeye akicheka. Pia ina tufanya kuwa na huzuni tukiona yeye akilia au akiwa na wasiwasi; katika amri wa chini kama huu. Na kwa hivyo sio kwamba sitaki yeye asikuwe na wasi wasi, au kwa sababu miye ni mchungaji. Sikutaka awe na wasi wasi kwa sababu nina mpenda sana, kwamba nina taka awe na furaha.

Nilipo tambua ya kwamba, Bwana alisema, “ Mwanangu, sasa unajua yale nina hizi kuhusu wewe. Sikuambia usiwe na wasiwasi kwa sababu ya kuto kuwa na wasi wasi. Nina kuambia usi we na wasi wasi kwa sababu nina kupenda sana na ninataka kuona ukiwa na furaha. Nina taka ufarahie maisha na, zaidi ya yote ufarahie upendo wangu maishani mwangu.”

Baba yako anataka maisha yako unayo ishi ya kujalisha sana, wewe furahia upendo wake na ulijua Yeye ana kuangalia wewe.

Wapenzi, Nina tumai kwamba hauta sahau yale Bwana aliniambia mimi. Baba wenu anataka maisha yako unayo ishi yasiwe ya kusumbukana, ukifurahia upendo wake na ukijua ya kwamba yeye ana kuchunga. Yeye anakupenda sana. Na upenda kamilifu – ukijua huu upendo makamilifu—utaweza kuondoa kila hofu maishani mwako (1 Yohana 4:18).

Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake au kuongeza dhiraa moja kwenye kimo chake? (Mathayo 6:27) Kwa hivyo msifadhaike mioyoni, wala msi ogope, na neema ya Mungu itatiririka kwa huru maishani mwenu, ikawasababishe nyinyi kuona Baraka zenu katika utajiri wake!

Hii naka imetolewa katika ujumbe “Neema Hutiririka Katika Eneo Huru Lisilotaabishwa Maishani Mwako” yaliyo hubiriwa na mchungaji Joseph Prince tarahe 17 Februari 2006.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Na: Joseph Prince

Joseph Prince is the senior pastor of New Creation Church — a dynamic and fast-growing church in Singapore, which has a congregation of 18,000 members. His ministry as pastor, teacher and international conference speaker focuses on unveiling Jesus and revealing His heart to the people.

Mengi Kuhusu Joseph Prince | Nakala iliyoandikwa na Joseph Prince