Sehemu ya 2: Kupumzika katika Yesu.

Na: Mike Walker
Kutoka: November 2009
Kupumzika katika Yesu ni ya kila mwamini wa Agano. Epu tuka shike hii ahadi ya Mungu.

Tukiwa na kukosa msimamo ulimwenguni na sauti zote zinazo nenea maishani mwetu, ni ya ajabu kupokea neema tele tele ya Mungu katika eneo la pumziko. Pale msalabani Yesu alilipa gharama yote kwa ajili ya amani yetu, kwa katika ukombozi wetu tuna ahadi ya pumziko.Kwa imani katika kazi iliyo kamilika Yesu aliyo fanya pale msalabani, mahala hapa pa pumziko, katika ukweli, ni amani kamilifu na ushindi katika kila eneo la maisha yetu na ina patika katika kuamini Injili!

Usiruhusu adui akudanganye wewe

Wabrania 4:1-3 “Kwa hiyo, kwa kuwa bado ahadi ya kuingia rahani iko wazi, tujihadhari ili hata mmoja wenu asije akaikosa. Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia, lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha,

Kunalo pumziko kwa watu wa Mungu.Kuna mahala ambako tunaweza kuishi na kujuwa kwa uhakika wa ajabu ya kwamba Mungu atafanya yale Aliyo sema Ata fanya. Kila kitu tunacho hitaji maishani mwetu na utaua inapatikana katika Kristo na katika kazi Yake ili kamilika ya ukombozi.Lakini kwa sababu ya kuto amini, watu wengi hawaamini, au hawawezi kupokea habari njema za Injili - amani, ushindi, uponyaji, ustawi, ukombozi na kila tendo jema. Zile nguvu adaui ako nazo maishani mwetu ni kutu ndanganya katika kuamini ya kwamba Injili sio kweli! Dini hutuambia ya kwamba yafaa tuifanyie kazi, ili Injili ya tuambia ya kwamba ni kuamini tu!

Pale msalabani Yesu alilipa gharama yote kwa ajili ya amani yetu, kwa katika ukombozi wetu tunayo ahadi ya pumziko.

2 Wakor 4:3-4 “Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea. Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu, ing’ae kwa wao.”

Wefe 4:17-18 – “Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 18Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao na ugumu wa mioyo yao.”

Hatutaki kutengwa kutokana na uzima tele tele ambayo Yesu alikuja kutoa, ila tuna taka kupumzika katika kazi iliyo kamilika ya Kristo. Amini ya kwamba Yeye ni kila kitu kinacho hitajika katika ushindi kamilifu maishani mwetu, maana tayari ameshinda ushindi, amekamilisha kazi na ameketi katika juu mbinguni. Tena ame tunia sisi juu kuketi pamoja na Yeye - sasa hii ni habari njema! Tunazo silaha zote za mbinguni tayari kushika nia yetu na kuamini Neno la Mungu, yaani Injili –“ Habari zilizo mzuri sana kuwa kweli, nab ado ni kweli”

Shida hizo ahadi za Mungu

Waebra 4:6 “Kwa hiyo kwa kuwa inabaki kuwa wazi kwa ajili ya wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii,” Jinsi nilivyo leta katika somo la kwanza juu ya “Pumziko”, Yoshua na Kalebu will amini report njema ya inchi ya ahadi na waka ingia ndani na kizazi kilicho fuata.Lakini kwa sababu ya kuto amini, tulikuwa na kizazi ambacho hakikuingia na kikafa katika jangwa.Kuna mahusuniko nyingi ambayo yata kuja kujaza akili zetu lakini tuna pigana “vita vema vya imani” na kushika amri ya ahadi ya Mungu.Tuna amani na Mungu inayo pita ufahamu wote na kuenda mbele katika ushindi maana tanajua shetani ako chini ya miguu yetu.

Amini ya kwamba Yeye ni kila kitu kinacho hitajika kwa ushindi ulio kamilika maishani mwetu maana tayari ana ushindi, kazi iliyo kamilika na ameketi juu mbinguni.

Waef 1:3 -“Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo.”

Waef 1:12-13 –“Ili kwamba, sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu Wake. 13Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia Neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa mhuri, kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi mliyeahidiwa,.....”

Neno la Ukweli ni habari njema ya wokovu.Kwanza sisi husikia habari zilizo mzuri sana kuwa kweli- sisi tume okoka na tuna ushindi katika kila eneo ya maisha yetu- na sasa tunapaswa kuiamini.Kwamba imefanyika, na sasa tuna tulia katika kazi iliyo kamilika ya Kristo - huru toka kwa dhambi, ugonjwa, tamanio, utumwa, umasikini, na kazi zote za shetani. Huu ndiwo uzima tele tele umbao Yesu alikuja kutoa, na nasi tumeketi juu sana ya usultani, nguvu, utawala, na nguvu na kila jina litajalwo!

Tumewekwa Mhuri na Roho Matakatifu

Waef 1:13 ina endeleah hivi “ ….Mkiisha kuamini, ndani yake mlitiwa mhuri, kwa yule Roho Mtakatifu wa ahadi mliyeahidiwa,” Tunapo amini Injili , tuna wekwa mhuri kwa Roho Mtakatifu wa ahadi. Mhuri ni alama , au mhuri au alama ya siri. Kwa mfano, inategemea nchi tunazo tembelea, tuna enda ng’ambo tuna pasi inayo hitaji mhuri wa siku za kuishi katika hiyo nchi tunayo tembelea. Iwapo hauna pasi basi hauwezi kuruhusiwa kuinga au kuondoka katika nchi. Maika michachi zilizo pita, mke wangu Jane na mimi tulikuwa safarini kuelekea Nigeria, Africa magharibi, kupitia London. Tulipo fika pale uwanja wa ndege wa Heathrow kule London, kijana moja wa Amerika ilikuwa kama amepoteza pasi yake, licha ya kushindani na wao na kupiga kilele, hakuweza kurusiwa kuingia na akarudisha Merikani.
Vivyo hivyo, Yesu ndiye pasi na kuamini ndiyo visa!Tunapo sikia ahadi na kuamini Neno la Kweli, tunaruhusu mhuri kuwekwa juu yetu- msamaha wa dhambi, uponyaji, mahitaji kupatikana, mwongozo, amani, urafiki, na ushindi mkubwa juu ya nguvu zote za adui! Tunayo alama ya mbinguni juu ya maisha yetu kwa kuamini Neno na kwa kuamini kazi zilizo kamilika za Kristo.

2 Wakor 1:20-22 inatangaza ya kwamba “ kila ahadi za Mungu ndani mwake ni ndiyo na amina.” Tunawekwa mhuri “…. Na tumepewa arabuni ya Roho ndani ya mioyo zetu.” Mungu ameweka mhuri Wake kuturidhi sisi juu yetu na Ameweka Roho Wake ndani ya mioyo kama hasina, inayo hakikisha kinacho kuja! Tunapo pumzika katika neno kwamba ahadi za Mungu ni zetu na ni sasa.

Na: Mike Walker

Rev. Walker along with his wife Jane set out to establish and build a strong local church in Post Falls, ID. Thus came the pioneering of Faith Tabernacle Church. Since that step of faith 23 years ago, this journey has seen them into over twenty countries.

Mengi Kuhusu Mike Walker | Nakala iliyoandikwa na Mike Walker