Amani na Ukarimu

Na: Peter Youngren
Kutoka: December 2008
Patikana ndani ya: Injili ya Neema
Maneno “Amani na Ukarimu” ni yanayo julikana kwa kila moja anaye hadithi ya Kikristo.Katika nakala hii Peter Youngeren anaangalia umuhimu uliyo nyuma ya maneno haya.

Je umewahi kushangazwa kuhusu ujumbe wa jeshi la malaika kule Bethelehemu, “Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu aliopendezwa nao!”
(Luka 2:14). Je ”amani na ukarimu” ya maanisha nini? Hii inaweza kuwa mojawapo ya mistira ya Bibilia zinazo kosa kueleweka.

Je malaika walipendekeza ya kwamba tokea wakati wa Yesu kuja watu wataweza kuishi kwa amani? Iwapo ni hivyo, kuja kwake Yesu basi ni kwa kukosea, jinsi tume jua aina ya vita vingi kwa miaka 2000 iliyopita.

Je wali dai ya kwamba Mungu atawapa amani wale watu wa ukarimu? Hii ingemaanisha injili yetu ni ujumbe wa matendo ya wanadamu na nguvu za kibinafsi:hakuna neema hata kidogo. Je wowote angefaulu? Ninani aliye onyesha ukarimu mwingi kupata amani ya Mungu? Je kuna yeyote kati yetu asiyekuwa na dhambi? Je si kila kinywa kimekoma? Je si kila mtu ameonyeshwa anechafuliwa na dhambi? (Warumi 3:19 ).

Katika mashindano yaonekanao, Yesu anasema, “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga” ( Mathayo 10:34) Katika sura ya inje kuna onekana mashindano. Je ni yapi? Kwa kushiriki neno la kweli sawasawa, tuna weza kupata jawabu kwa urahisi kwa hili swali.

Vita vya Mungu na dhambi za mwanadamu zimekwiisha!

Kwa kweli, Mungu anataka amani miongoni mwa watu, lakini huu haukuwa ujumbe wa kimsingi wa jeshi la malaika. Semi, “amani na ukarimu” Ina dhirisha moyo na makusudi ya Mungu kuelekea watu. Mungu alikuwa na vita na dhambi za mwanadamu tangu bustani ya Edeni. Na sasa vita vimeisha! Chanzo cha mashindano kati ya mwanadamu na Mungu (dhambi) imeweza kuondelewa na mwokozi.

Mungu hakujificha toka kwake Adamu-ila Adamu alijificha mwenyewe toka kwake Mungu.

Mungu amewapenda watu kila wakati, jinsi inavyoonekana Adamu alipo fanya dhambi. Mungu hakujicha toka kwake Adamu - ila Adamu alijificha toka kwa Mungu. Mungu ni mchungaji wa milele, mchungaji mkuu anaye tafuta kondoo aliyo potea. Kurasa chache katika kitabu cha Mwanzo, tunamwona Kaini, muuaji wa kwanza. Kinyume chake Mungu alimfikia Kaini hata alipo danganya kuhusu kifo cha nduguye. Je kwa nini Mungu hakuweza kugeukia muuaji and mhongo mgongo wake. La Mungu ana wapenda wenye dhambi; kila wakati Amefanya hivyo. Kaini alipotambua alipatikana ali mwomba Mungu amlinde. Je Mungu anaweza kulinda muuaji? Kwa kushangaza jawabu ni “ndiyo”, baadaye tunasoma, “Kwa hivyo, Kaini akatoweka wepo wa Mungu” (Mwanzo 4:16) Hauwezi kuwacha usijo kuwa nacho. Mungu hakumwacha Kaini – ila Kaini alitoweka Mungu. Tena tunaona upendo wa Mungu kwa ulimwengu wa dhambi tangu mwanzo.

Haya na nakala zingine zinatuonyesha kwamba Mungu alikuwa ni “kama haoni” (Matendo 17:18), akijua ya kwamba adhabu ya dhambi mwisho wake ni katika mwili wa Yesu. Japo tulikuwa na hali ya kutokuwa na uhakika. Wakati wa kipindi kati ya Adamu na Musa, Mungu aliadhibu dhambi wakati kizazi kilichoendele chote kilikwa katika hatari, kama ile hali ya wakati wa Nuhu. Bado wakati mbaya mno, Mungu aliweza kutoa nafasi za kutoa sadaka na dhabihu za ondeleo la dhambi.

Katika kipinda na majira ya kati ya Musa na Yesu, sheria ilikuwa ikitenda kazi kwa watu wa Israeli. Sheria haikutolea kumfanya mtu yeyote matakatifu, au kuwa ndicho kipimo cha mwandamu kuishi.Ila makusudi ya sheria ilikuwa ni kuonyesha utakatifu wa Mungu na utupu wa uweza kufikia hali yake Mungu. Sheria ilikuwa ituandaye kwa Neema. Kipindi cha mika 1400, kipindi kinacho itwa Agano la kale, tulikuwa na hali ya hasira na gadhabu. Mara kwa mara dhambi, dhambi zili adhibiwa jinsi watu wa Israel wilikosea kushika amri za Mungu.

Hi yote ni kurudia ujumbe wa malaika : amani, ukarimu kuelekea wanadamu.” Mara tu tunapo elewa sheria ya Musa, pamoja na masharti yake yote yasiyo wezekana, pia tunaelewa Agano Jipya la amani.

Vita visha isha. Amani ilikuja. Yesu kwa uhakika sasa anaweza kudhirisha Mungu kama vile baba hukumbatia na kupuzu.

Je ni upi ulikuwa msingi wa amani hii? Kwamba Yesu Kristo ange weza: “mara moja hata milele” kukabili shida ya dhambi. Mungu angetendea dhambi kile dhambi ilihitaji na yale Mungu kila wakati alitaka kuyatenda – kuadhibu dhambi. Hasira ya haki ya Mungu ilianguka juu yake Yesu. Vita vikakwisha. Amani ilikuja. Na sasa Yesu mfafanua Mungu vile baba anakumbatia na kupuzu.

Kwa nini Mungu anabadilisha toka Agano la kale kuelekea jipya?

Je Mungu amebadilika?

La hasha! Mungu alikuwa makatifu, mwenye, haki, safi na tayari kupata kuadhibu dhambi. Tofauti ni kwamba sasa adhabu tayari imewekwa kwa Yesu, matokeo yake ni ujumbe wa amani na ukarimu toka kwa Mungu. Kwa ufupi, dhambi zako zimeshalipiwa. Usimfanye Mungu kuwa wa kuhukumu, Mungu wa kulipa kisasi kana kwamba hawezi kushiriki na wenye dhambi. Wengine wana onyesha Mungu kuwa Mungu mkali, ambaye analipwa fedha kwa utungu. Sisi “hatulipi” katika maombi, kutoa, kushirika katika kanisa na matendo mazuri kumfanya awe na furaha. “Amani na ukarimu inamaanisha ya kwamba Mungu haitaji kuridhishwa. Yeye ameridhika na dhabihu Yesu aliyetoa. Hii haifanyi dhambi kuwa nyepesi. Yohana anaandika, “Basi, kila mtu aliye na tumaini hili katika Kristo, hujiweka safi kama vile Kristo alivyo safi kabisa.” (1Yohana3:3 ). Unapo amini katika tumaini la Injili, kwamba Kristo “mara moja hata milele” amelipia dhambi zako, inakupa mzukomo wa kuwa safi. Mungu hakupuuza dhambi. Alizilipia na kuziondoa njiani mwetu.

Kama kunakitu, kifo cha Yesu msalabani ni kulipa zaidi za dhambi za wanadamu.

Yohana mbatizaji aliunga mkono ujumbe wa malaika.
”Semeni na moyo wa Yerusalemu, kuambieni kwa sauti kuu ya kwamba, vita vyake vimekwisha, uovu wa wake umeachiliwa ; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa zake zote” (Isaiah 40:2) Kila hali ya vita kati ya Mungu na mwanadamu vimekwisha kusudi ya dhambi zimelipiwa marudufu. Huu ni msemo waajabu unao onyesha kwamba hakuna mtu atakaye fikiri ya kwamba dhambi zao hazikulipiwa kikamilifu. Kama kunakitu, kifo cha Yesu msalabani ni kulipa zaidi kwa dhambi za mwanadamu.

Agano la Amani

Isaya alitabiri ujumbe huo huo: “Maana milima itaondoka, vilama vitaondelewa:bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa, asema BWANA akurehemuye” (Isaya 54:10) Ahadi ya Mungu ya “amani na ukarimu” ni isiyobadilika. Ujumbe wa Isaya unaingiana na ule wa Yohana Mbatizaji pia ule wa malaika. Yesu kuja kwake alianzisha agano la amani ambalo ni la milele.

Isaya sura ya 53 inaeleza katika undani ile gharama ililipwa kwa ajili ya agano la amani. Mwili wa Yesu uliathirika mno “uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote” (Isaya 52:14). Hakujichukulia kanuni ya dhambi juu yake Mwenyewe, ila kwa ukamilifu ya uovu wa mwanadamu. “Hakumu ya amani ilikuwa juu Yake … Bwana aliweka juu Yake dhambi ya sisi sote.” Mungu aliweka dhambi za binadamu juu ya mwili waYesu ili aweze kuweka haki ya Yesu katika kila mtu aaminiye.

Yesu alitezwa katika kila ubaya, dhihaka na matendo ya meteso ambayo hauzi kufikiri juu ya mwanadamu. Kila hatua ya kuwa kwake ili athirika – kimwili, kiakili na kimawazo. Kuzaliwa kwa Yesu kulionyesha amani na ukarimu: ile 1400 maika ya sheria ya Musa ilikuwa juu ya Israeli ilikuwa imekwisha. Kwanzia sasa na kuendelea wema wa Mungu utaleta watu katika toba (Warumi 2:4)
Jugumu letu ni kushiriki ujumbe wa amani toka kwa Mungu. Na jinsi Injili ya amani inapo badilisha mamilioni ya maisha hya watu tuta pata amani miongoni mwa watu.

Na: Peter Youngren

As founder of World Impact Ministries, Celebration Bible College, Way of Peace and the Celebration Churches in Toronto, Hamilton and Niagara, Canada, Peter is committed to equipping believers to fulfill their purpose before the return of Jesus Christ.

Mengi Kuhusu Peter Youngren | Nakala iliyoandikwa na Peter Youngren