Amani Nyakati za Hatari

Na: Mike Walker
Kutoka: April 2009
Patikana ndani ya: Injili ya Neema
Uvumi huja kutuweka katika hofu, lakini Yesu tayari ametupa amani Yake!

Inaonekana kana kwamba kokote tunapo angalia leo hii Hajalishi ni wapi twa geukia, kuna habari mbaya zina kuja. Swali linaweza kuja niani mwako: “Je kuna nini ina Endelea?”

Nina habari njema kwako leo hii na hiyo habari njema ni Injili ya Yesu Kristo - Injili ya neema. Pale msalabani Yesu alilipa gharama yote kwa ajili ya amani, kwa hivyo nina andika kukuimiza wewe katika nyakati hizi za hatari ambazo una ishi ndani!

“Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari.” (2 Tim 3:1)

Tuna jua tupo katika nyakati za mwisho maana Bibilia ina nakili maneno ya mtume Petero katika Matendo 2:17 ambako alitangaza: Hivi ndivyo ilivyo nenwa na nabii Yoeli,  kwamba siku za mwisho nita mimina roho wangu kwa kila mwilli.” Kwa hivyo kupitia semi hii tuna elewa tumekuwa tuki ishi katika siku mwisho kwa miaka 2000. Kwa kila habari na taarifa tunazo shuhudia katika runinga au tunasoma katika magazeti, tuna jua tuna ishi katika nyakati za hatari.

Neno hatari lina maanisha: hatari, ngumu, kubeba, hatari mno au hatari kabisa. Nina fikiri hii maelezo sawasawa ya yale tuna ona katika ulimwengu sasa hivi. Ndiyo, tuna amini katika agano la neema ambalo Yesu alilitia nguvu kwa umwagikaji wa damu Yake pale msalabani. Tuna amini habari zilizo mzuri sana kuwa kweli, lakini ni kweli. Lakini kweli ni kwamba kila siku tuna pigwa na kombora la sauti ya hofu. Kwa hivyo katika hii nakala ninaleta ili tuondoe silaha ya hofu na kukutia wewe maishani na amani na upendo wa Mungu!

Bibilia inatuambia sisi katika Agano Jipya andiko lina patikana katika Warumi 15:4: “Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.”

Wakati linapo ongea kuhusu “mambo” haya lina ongea kuhusu mambo katika Agano la Kale na jinsi yalivyo vivuli ya jambo la kweli - ambaye ni Yesu yeye mwenyewe! Zaidi ya yale tunaona katika Agano la Kale ni yale tunaita “aina na vivuli” ya mambo tunahitaji kuona maishani mwetu leo hii. Tunaweza kujifunza kutoka kwayo na tena kufahamu, tuna weza jifunza jinsi ya kuishi katika uweza wa Agano Jipya leo hii! Kumbuka hizi ni vivuli tu….Yesu ndiye kweli na tunapo mwona Yesu, basi vivuli vita leta maana.

Uvumi huja na kusudi moja na ni kutufanya sisi kuwa na hofu na kutushusha sisi kama watoto wa Mungu.

Sasa tuna taka kuchukua somo la vivuli na tupitilishe mpaka kwa msalaba na yale Yesu alizungumzia. Na hapo tuta ona jinsi inatuhusu katika maisha yetu ya kila siku. Hii ni njia moja tunaweza kupata nguvu kutoka kwa Neno la Mungu na tufahamu ya kwamba Mungu hakuweka kitu chochote katika neno lake kimakosa. Iko pale kwa sababu fulani tuishi uzima ule Yesu alikuja kutoa. Katika Agano la Kale, Nabii,Yeremiah, anafunua ukweli mkubwa kwetu sisi kuhusu maisha yetu sasa na kwangu mimi ni ya kuhimiza sana. “Msikate tamaa wala msiogope tetesi zitakaposikika katika nchi, tetesi moja inasikika mwaka huu, nyingine mwaka unaofuata, tetesi juu ya jeuri katika nchi na ya mtawala dhidi ya mtawala.” (Yere 51:46)

Tambua ya kwamba Bwana ana tufunulia kwetu sisi kwamba kuna uvumi unatungojea sisi kila mwaka- mwaka mpya, uvumi mpya, mwaka baada ya mwaka. Imekuwa hivyo kila wakati na itaendelea kuwa hivyo, na Bwana anatupa mambo ya vilindi hapa, na tujue ili tusi ishi katika hofu. Uvumi huja na kusudi moja, na ni kutufanya sisi kuogopa na kutushusha sisi kama watoto wa Mungu.

Maana iwapo adui akitupata kama watu wa Mungu kuishi katika hofu na kukata tamaa, basi ni vipi giza litakuwa giza kuu?Iwapo tuna ogopa, ni kwa kuogopa kiasi gani watu watakuwa? Mungu anaruhusu sisi tujue uvumi, uta kuja kila mwaka kushusha agano la watoto wa Mungu. Uvumi huja kupita vyombo vya habari na vyombo vingine na kazi yake ni kutuweka katika hofu na kutoa katika Neno la Mungu.

Yesu alituambia katika Yohana 14:27 “Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.”
Kutoka kwa kinywa cha Yesu: MSIFADHAIKE MIOYONI MWENU WALA MSIOGOPE!” Yesu tayari ashawapeni na kwangu mimi amani Yake; tunahitaji kuondoa fadhaa iwe inje ya moyo. Amani tayari iko hapa; iko ndani yako wewe unaye amani- wewe ondoa fadhaa!

Yesu tayari asha kupa wewe na mimi Amani Yake; tunahitaji kuondoa fadhaa iwe inje ya moyo.

Yesu alisema, “Amani yangu nawapa,” kwa hivyo hauhitaji kuomba kwa ajili ya amani- amani iko ndani yako wewe unaye amani! Kama mtoto wa Mungu, amani ni yako. Amani maana yake ni kukosekana machufuko! Na tusi changanyikiwa na kusahau sisi ni akina nani na Mungu wetu ni nani! Na tusi sahahau ni kwa wingi gani Baba yetu anatupenda na kwamba mwanawe Yesu, alilipa gharama yote- tuna agano la neema!

Yesu angali anajenga kanisa leo hii na sisi ni kanisa. Yesu alisema, “ Nina wapa amani Yangu.” Amani pia ina maanisha afya, wema, kustawi na kila aina ya wema! ndiyo kuna uvumi nyingi leo hii na habari mbaya mno huja. Kuna uovu mwingi katika ulimwengu, walakini kuna mema nyingi! Mtume Paulo anatuimiza sisi Waru 12:21 “Usishindwe na ubaya, bali uushindeni ubaya kwa wema.” Wema utashinda ubaya, nuru kila wakati inashinda giza, amani katika habari njema za Yesu Kristo. Alisema kwetu sisi, “ amani nina wawachia” Hii pia ina maanisha kuenda mbele; ina maanisha baraka zote zinazo ambatana na kutiririka kutokana na upatanishi wetu na Mungu!

Yesu alisema, “ amani nina wawachia”… mambo haya yote nina wawachia- ni mibaraka zote zinazo kuja wakati wewe umepatanishwa na Mungu. Yesu alilipa gharama yote ya dhambi. Yeye alitupatanisha sisi na Mungu kwa hivyo tuna amani na Mungu. Yesu aliye kuwa tajiri mbinguni alifanyika masikini ili kwamba tupata mapato. Pale msalabani alichukuwa magonjwa yetu yote ili tuishi katika afya. Yeye alikataliwa na rafiki Zake wote ili kwamba tufanyika marafiki yeye. Alichukua machafuko yetu yote ili tutembea katika hekima. Yesu kwa ukamilifu alishinda nguvu za giza ili tuishi katika ushindi maishani mwetu.

Mtume Paulo anatupa mtizamo wa nguvu katika ukweli huu katika 2 Wakori 5:17-21; “Kwa hivyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupatia sisi huduma ya upatanisho: Kwamba Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi Yake mwenyewe, na hawezi kuhesabia watu dhambi zao tena. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa vyetu, nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. Kwa maana Mungu alimfanya Yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu katika Yeye.”

amani nina wawachia kwa hivyo msiogope chochote

Mungu hana uwazimu kwa ajili yako; Yeye hatafutii njia ya kuumiza wewe. Yeye hataki kukuadhibu wewe;Yeye haja kukasirikia wewe- kuna amani kati yako na Mungu!Wewe umepatanishwa kwa neema ya ajabu ya Mungu. Yesu alichukuwa dhambi zetu na adhabu yetu ambayo hakupaswa na akatupa sisi haki ambayo hatukupaswa kupata!Sisi tume patanishwa!

“Amani nawaachia, amani yangu nawapa, amani hii niwapayo si kama ile ulimwengu utoayo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.” (Yoha 14:27)

Ndiyo kuna uvumi unao tungojea sisi hata hivyo mwaka huu. Uvumi unatumwa kwa ajili ya kusudi moja ni kwamba tukate tama au tuwe na hofu. Kunaweza kuwa na uvumi mwingi unakuja, pia tunazo baraka! Inawezakana tukawa na uvumi wiki ijayo, walakini pia tunayo baraka wiki ijayo. Yesu alisema, nina wawachia nyinyi amani yangu; nina wawachia baraka zote ambazo huja wakati umepatanishwa na Mungu. Kwa hivyo misfidhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Tafsili yake katika Kiyunani ni usi ogope chochote . Yesu, mkombozi wako, ananena na moyo wako: amani nina wawachia ili usi ogope chochote. Yesu alisema, “ Nime wapa ninyi kutokuwepo kwa machufuko, afya yangu, mali yangu, vitu vyangu vema; baraka zangu zilizopo na baraka zangu za usoni nime wapa ninyi ili kwamba usikuwe na hofu na chochote.” Neema teletele ya Mungu hutupa ukweli wa amani katika nyakati za hatari!

 

 

 

Na: Mike Walker

Rev. Walker along with his wife Jane set out to establish and build a strong local church in Post Falls, ID. Thus came the pioneering of Faith Tabernacle Church. Since that step of faith 23 years ago, this journey has seen them into over twenty countries.

Mengi Kuhusu Mike Walker | Nakala iliyoandikwa na Mike Walker