Kupumzika ndani ya Yesu (sehemu Tatu)

Na: Mike Walker
Kutoka: December 2009
Patikana ndani ya: Injili ya Neema
Maisha na Bwana yafaa yawe ya kutulia .Ni vipi tunaweza kumtumikia aje Bwana nab ado tuwe watulivu?

Sisi, ambao tuko katika hili Agano Jipya ambalo Mungu ametupa kupitia Yesu Kristo, tunalo tunuko la kuhishi maisha tulivu, pasipo mzongo pamoja na Mungu. Kwa watu wengi hii kweli ina onekana iko mbali sana kwa sababu machafuko ndani na yaliyo zunguka maisha yao. Yesu angali analeta amani katika dhoruba la maisha yao. Kuna pumziko, linalo onekana la kweli kwa watu wa Mungu! Kuto amani huleta mzongo na kutotulia, lakini kuamini katika kazi iliyo kamilika ya Kristo huleta pumziko.

Kutoamini huleta mzongo, na kutotulia, ila kuamini katika kazi iliyo kamilika Kristo huleta pumziko.

Waebr 4:1-4 “Kwa hiyo, kwa kuwa bado ahadi ya kuingia rahani iko wazi, tujihadhari ili hata mmoja wenu asije akaikosa. Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia, lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha, kama vile Mungu alivyosema, “Hivyo natangaza kwa kiapo katika hasira Yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani Mwangu.’ ” Lakini kazi Yake ilikamilika tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Kwa maana mahali fulani amezungumza kuhusu siku ya saba, akisema: “Katika siku ya saba Mungu alipumzika katika kazi Zake zote”.

Ufalme wa mbinguni niwetu

Tunaweza kuishi na kutenda kazi katika angaa mpya ambako tutakuwa tume koma kutenda kazi zetu wenyewe.

Maisha yetu na Bwana yafaa yawe ya pumziko na sio ya tafani na upepo wa unao tupulizia toka pande zote. Tunaweza kuishi na kutenda kazi katika angaa ambako tume koma kutenda kazi zetu (Webr4:9) na kujua ya kwamba kila hadi ya Mungu yetu maana Kristo alitimiza kila ahadi na ameketi chini kwa mkono wa kuume wa Mungu. Tuna weza sema kwa ujasiri tunajua nina tume mwaamini na tume shawishika ya kwamba Yeye anaweza kutimiza kila tume mpa Yeye (2 Timoth1:12)

Ufalme wa mbinguni ni wetu kupitia Kristo- tume pewa sisi.

2 Petero 1:3 ”Uweza Wake wa uungu umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu, kwa kumjua Yeye aliyetuita kwa utukufu Wake na wema Wake mwenyewe.” Mungu wetu ni mwema na Ame tupa kila kitu kinacho hitajika kwa maisha yetu na uungu kupitia Kristo Yesu. Tuna hekima, amani, haki na kila ahadi zilizo zaidi za thamana kitika Bibilia zilizo wekwa juu yetu.

Fanya kazi kuingia katika raha Yake

Wabra4:11- ” 11Basi na tufanye bidii kuingia katika raha hiyo, ili kwamba asiwepo ye yote atakayeanguka kwa kufuata mfano wao wa kutokutii.” Kuna watu wengi walio na mzongo katika Ukristo walio shindwa kuelewa na kushika ya kwamba wakati unaye Yesu, tuna kila kitu! Yesu yu nasi kila dakika ya kila siku na Yeye anatosha kwa ya kesho na siku za usoni. Watu wengine wanahitaji mikono kuwekwa juu yao na neno la unabii, lakini tunahitaji kuamini katika Yesu kila moja wetu - Yule ambaye hawezi kutuwacha au kutu tupa!

Kuna mahala tunaweza kukimbilia, ile mbio iliyo wakwa mbele zetu bila kuchoka na moyo unao zimia.

Isaya 40:29-31 ”Huwapa nguvu waliolegea
na huongeza nguvu za wadhaifu. 30Hata vijana huchoka na kulegea,nao vijana wanaume kujikwaa na kuanguka,
31bali wale wamtumainio BWANA atafanya upya nguvu zao.Watapaa juu kwa mbawa kama tai,watapiga mbio wala hawatachoka,watatembea kwa miguu wala hawatazimia.”
Kuna mahala tunapo weza kukimbilia pasipo kuchoka na kuwa na moyo unao zimia.Katika 1 Wakor 15:10 Paulo anasema ya kwamba Alitenda kazi sana kuliko wote” lakini ilikuwa ni neema ” neema ya Mungu iliyo kuwa na mimi.” Lengo lake katika hudumu ilikuwa mahala pa kupumziko ambako aliwezezwa na Bwana.Yesu alikamilisha ile kazi ambayo Baba amenipa kumaliza” (Yohana 5:56). Alisema na kufanya yale baba alimwambia Yeye kufanya na aka tulia kwa ukweli.Alijua njia ya Baba alikuwa nayo kwa ajili Yake kufuata na akatulia katika matokeo ya kilicho wekwa mbele zake.

Lengo lake katika huduma ilikuwa ni mahala pa pumziko mahala kazi iliwezezwa na Bwana.

Waef 2:10 ” 10Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.” Tunahitaji kuenda, mbele katika vitu ambavyo vime andaliwa mbele zetu. Tunahatiji kumakinika kwa Roho Mtakatifu na kudumu katika mpango wa Baba. Tole kila kitu jinsi ulivyo na pata Bwana na ata tuongoza bila mzongo na bila ukosefu wa ushauri wetu. Iwapo hatuna uhakika wa kuenda mbele wenyewe katika kufanya mashauri, usi ende mbele. Yesu ni Bwana wa maisha yetu na tunahitaji kusikiliza yale Anaye sema.

Tunahitaji kumakinika kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu na kudumu katika mpango wa Baba.

Tunefunishwa nira na Bwana

Mathew11:28-30 ” 28“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.’’Maisha ya Kristo madhumuni yake ni kukuwa ya kupumziko, au yasiyo kuwa na mzongo. Hakuna nafasi kwa huduma ya waliyo choka katika kumtukia Bwana. Tunapokuwa tunafanya kazi kamili kwake Yesu, hatuwezi kuchoka maana hatufanyi katika nguvu zetu wenyewe. Tunafanya kazi ambao Bwana ametuandalia:kazi ambayo ametuandalia sisi. Ni tofauti gani tuliyo nayo wakati tume funganishwa na Bwana - Yeye ndiye ana vuta mzigo mzito na sio sisi! Hii maisha teletele pasipo kuwa na mzongo, ambayo ni uzima Yesu alikuja kutoa. Jawabu la mzongo ni: Njooni mjifunze kwangu!

 

Na: Mike Walker

Rev. Walker along with his wife Jane set out to establish and build a strong local church in Post Falls, ID. Thus came the pioneering of Faith Tabernacle Church. Since that step of faith 23 years ago, this journey has seen them into over twenty countries.

Mengi Kuhusu Mike Walker | Nakala iliyoandikwa na Mike Walker