Wokovu Waishi Ndani Yako

Na: Scott McIntyre
Kutoka: September 2008
Patikana ndani ya: Kristo ndani yako
Yesu sio tu mtoaji wa wokovu. Yeye ndiye wokovu.

Je una furaha ya kuokoka? Kwa uhakika ninayo furaha. Hakika ukiuliza kila Mkristo iwapo yeye ana furaha ya kuokoka, jawabu litakuwa “ndiyo”. Walakini, ukiuliza kila mkristo uokovu ni nini, kwa uhakika utasikia majibu kwa wingi. “ Wokovu una maanisha nita enda mbinguni nitapo kufa ;” “ wokovu ni uhuru toka kwa dhambi”. “ wokovu ni ukombozi… Uponyaji… Uhuru… urejesho… ukamilifu… hifadhi”. Ndiyo, haya yote ni majibu mzuri sana. Lakini ni nusu kwa uzuri.
Wokovu ni Mtu

Wokuvu ni nini? YESU. Bila yeye, hakuna baadhi ya vitu vilivyo tangazwa awali vipo kwa ajili yetu. Walikini na Yeye, vyote vile vitu vuzuri ni vyetu sasa, pamoja na baraka zingine toka kwa Mungu. Yesu sio tu mtoaji wa wokovu. Yeye ndiye wokovu. Epu sema haya kwa sauti pamoja nami: “Yesu ni wokovu wangu “.

Karne nyingi kabla kuja kwake Kristo katika mwili, nabii Isaya alikuwa na mengi ya kusema kuhusu Yeye. Angalia maneno haya kutoka kwake Isaya 49:6 ambayo Mungu ana mnenea Masihi: “naam, asema hivi, ni neon ndogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila zote, na kuwarejesha watu wa Israel waliohifadhiwa,zaidi ya hayo, ni nita kutoa uwe nuru ya mataifa,upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.”

Je unaweza kuona ya kwamba? Mungu alimtuma Yesu KUWA wokovu. Mungu hakusema ya kwamba Yesu atatoa tu wokovu. Hakusema Yesu atawawekeya viwango kwa wanao tarajia kuongoka. Wala hakusema kwamba Yesu atafundisha njia liyo bora ya kuokoka. Mungu alisema Yesu ATAKUWA wokovu. Hiyo ndiyo habari njema kwetu sisi, rafiki yangu. Wokovu hauhitaji ukamilisho, kana kwamba Mungu alifanya ingine sehamu tu au kiasi, na kwamba ipo juu yetu kukamilisha. La, kwa Myahudi na myunanni Wokovu uko hapa. Jina lake ni Yesu.

Nina penda yale Mungu alisema katika fungo lilo nukuliwa hapo juu. Ndiyo Yesu alikuja kwa ajili ya taifa ya Israel. Shukuru Mungu kwa ajili ya upendo wake kwa Wayahudi. Lakini hakukomea pale. Kutumia Kingereza cha kisasa, Mungu alisema, “ Hiyo haitoshi. Nina penda Israel nami nita warejesha wao. Lakini hiyo haitoshi Yesu, utakuwa wokovu Wangu kwa kila mtu.”

Tangia hapo mwanzo, mpango wa Mungu ulikuwa katika utendaji (Ufunuo wa Yohana 13:4) Yesu alikuwa wokovu wa kila watu.

“Usi sahau Kuhusu Simioni “

Nina jua hii ni barua ya habari njema ya mwezi wa Tisa, lakini tunahaitaji kuona Ushuhuda wa tabia katika yale huwa tunaita hadithi ya Krismasi. Hata tangu nilipo anza kuona Kuwa Yesu ni uwokovu wetu, wazo languy kuhusu hadithi hii ni kwamba “usi sahau kumhusu Simioni”.

Luka 2 ina nakili ya kwamba Roho mtakatifu alikuwa amefunulia Simioni ya kwamba hata kufa kabla ya kumwona aliye Bwana Kristo. Sawa, siku ikafika mwishowe ambako Mariamu na Yesufu wsalimleta yule motto Yesu ndani y a hekulu kulingani na desturi za Kiyahudi. Simioni pia katika mwongozo wa Roho, alikuwa hekaluni siku hiyo, akikutana na Mariamu na Yusufu aliwezezwa kumshika motto Yesu mikononi mwake. Hapa kuna yale Simioni alisema alipokuwa ana mshika motto Kristo mikononi mwake. “ Sasa, Bwana wamruhusu mtumishi wako, kwa amani,kama ulivyo sema; kwa kukua macho yangu, yame,uona wokovu wako…. “ (Luka 2:29-30)

Je Simioni “ alikuwa ana ona kitu katika Roho?” La. Alikuwa anaona motto mvulana. Lakini alitangaza ya kwamba mtoto aliye mikononi mwake ni alikuwa ni wokovu wa Mungu kwa watu wote. Ni ajabu kutumbua y akwamba Simioni alisemekana alikuwa tu “ mwenye haki na mcha Mungu.” (Luka 2:25 ). Lakini katika kusoma maneno yake, tunaweza kuona ya kwamba ujasiri wa hakukua katika uchaji wake. Tumaini lake lulikuwa katika Yule aliye wokovu. Nina furaha kufuata mfano wa Simioni, nina tumai, hata wewe vivyo, Ni vema kujitolea kwa Mungu katika shauku la kumpendeza Yeye. Walakini usi weke imani yako katika unayo weza, au kufanya. Imani ni ya Yesu pekee yake.

Tumaini la Simioni halikuwa katika uchaji wake. Tumaini lake lilikuwa katika yeye aliye Wokovu.

Tambua Tena Furaha na raha ndani ya Yesu

Labda umekuwa uking’ang’ana kupendeza Mungu, au unang’ang’ana kupata kitu toka kwa Mungu. Huenda umepungukiwa kuhusu usiano wako na Mungu. Au kwa njia ingine ume amua ya kwamba baadhi ya baraka za Mungu ni watu wengine na sio zake wewe. Labda wewe ni muhudumu kikamilifu, lakini hauoni matokeo ambayo umetarajia na unajiona kuwa umeshindwa.

Niruhusu kushiriki mifano michache, ambazo nina amini zita kusaidia kutumbua tena furaha na raha ndani ya Yesu, aliye wokovu wake. Ukweli na usemwe, wakati mtizamo wetu ni kwetu sisi tuta shindwa na hali, mara nyingi kuliko itupasavyo. Lakini tunapo mtazama Yesu, tuna tulizwa, tiwa nguvu na kujazwa imani yake.

Kufungua Karama ya wokovu

Je umewahi kupokea kipawa kilicho funikwa vizuri katika kijisanduku. Natumai umewahi maana kupokea kipawa ni jambo la kufana sana. Na sasa unapo pokea kipawa unafanya nini? Je unapobeba kipawa kimefungwa vizuri, uta onyesha kila mtu anaye kutana naye? La. Je uta weak kipawa hicho kwa mezani pale ili uweze kuangalia tu jinsi lkilifungwa vizuri hata siku sijazo? La. Utafanya nini? Sawa! ukiwa kama mimi funguwa kifurushi hicho upesi sana! Ukitaka kujua kila kitu kilicho wekwa ndani na yule aliye toa. Oh, hiyo ni furaha na ya kufana sana.

Rafiki yangu wokovu ni kama karama kutoka kwa Mungu, na kimeletwa kwako katika ukamilifu wake kupitia aitwaye Yesu. Hauitaji kuomba, omba Mungu chochote, au usi fikirie wewe umetengwa kutokana na baadhi ya baraka za Mungu. Kitu cha kipeke ni kutambua zaidi,na zaidi ya yale tumepokea katika Yesu.

Hakika nikiandaa aya hii, nina kumbushwa maana ya Yesu, kuhusu kazi ya Roho Matakatifu Yohana 16:14.
Shukuru Mungu kwa ajili ya Roho Mtakatifu wake anaye tusaidia kufunguwa kipawa cha wokovu!

Tunapo soma Neno la Mungu na kusikia Neno lake likifundishwa, Roho Mtakatifu huonyesha sisi kwamba Haki na Utakatifu vimekuja kwetu kupitia Yesu. (Waefeso 4:20-24 ). Uponyaji na Ukamilifu ni wetu katika Yeye. Isaya 53:4-5, I Petero 2:24 kupokea mahaitaji yetu huja kupitia Yeye. ( Wafailipi 4:19) Neema na amani vimezidishwa kwetu katika kumfahamu Yeye. ( 2 Petero 1:2 Hii nakala inaweza kuenda mpaka kurasa nyingi, lakini kwa sasa nita sema kutambua ukuu wa Kristo, tunahuishwa kukubaliana na mwandishi wa kitabu cha Waebrania, anapo weka maelezo yake kushusu Kristo katika muhtasari, na semi iliyo rahasi… wokovu muku wa namna gain? Waebrania 2:3 a

Kisima cha wokovu ndani yako

Katika kutamatisha, Yu wapi Yesu leo hii? Yeye yupo ndani yako (Wakolosai 1:27) Hakika anathirisha uzima wako ndani mwako, katika yule mwamini kama chemichemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele Yohana 4:14. Sasa tukikumbuka ya kwamba Kristo yu ndani mwako, angalia huu muktadha kutoka kwa Isaya 12, ambako tuna pata ufunguo kupokea kutoka kwa Mungu na tukiwa chombo cha uzima wake.
“Tazama Mungu ndiye wokovu wangu, Nitatumaini wala sitaogopa; maana Bwana Yehova ni nguvu zangu na wimbo wangu, naye amekuwa wokovu wangu.”

Kristo ndani yako ni chemichemi ya ya wokovu, Je inamaanisha nini kwetu, Kuchota toka kwa kisima? Katika mtizamo wa kwanza, hii inaokena kama kazi nyingi. Iwapo unahitaji maji mengi, hiyo itahitaji nguvu zaidi kuibeba. Je Isaya anasema ya kwamba ipo ipo juu yetu kusababisha vitu kutendeka?La hasemi hivyo. Nina amini Isaya anasema tu furahie faida ya wokovu, katika njia moja tunapo chota maji yetu.Katika siku za Isaya watu walipata maji yao kwa kuteremsha chombo ndani ya kisima, alafa kuvuta hicho chombo juu. Je ni vipi kwako leo hii? Jew wewe huingia nyuma ya bustani ya kuteremsha ndoo ndani ya kisima. La, Badili yake, wewe huenda kwa bakuli la kuoshea vyombo na unafungua mfereji ; Hapo kuna picha ya ajabu kwako na mimi. Yesu ni, wokovu wako, ni kisima cha uzima wa Mungu ndani yako. Yeye ndiye haki yako, utakatifu wako,hekima, uponyaji na nguvu zako. Yeye ndiye upako ndani yako awezezae wewe kuhudumu. Na yote unayo hitaji kufanya ni kufungua mfereji uendelee kuwa wazi kwake.

Kando na Yesu, hatuwezi kufikia wema wa Mungu. Lakini Yesu akiwa hai ndani yetu, tunaweza ktambua na kutumia kila kitu ambacho Mungu ametupa ndani Yake. Yesu wokovu wako ni kisima cha uzima wa Mungu ndani yako. Yesu ni wokovu wako.

Hauhitaji kulipia kilipia kisima hicho. Hauhitaji kuchimba hicho kisima, hauhitaji kuweka pomba, au mfereji. Tumbua Yesu yu hai ndani yako, na ufungue mfereji kwake.

Na: Scott McIntyre

Founder of Front & Center Ministries
Ontario, Canada
http://www.front-and-center.ca

Mengi Kuhusu Scott McIntyre | Nakala iliyoandikwa na Scott McIntyre