Tuangalie Upya Kwake Yesu.

Na: Peter Youngren
Kutoka: August 2009
Peter Youngren ha jaribu kutubadilisha watu kutoka dini moja had ingine , ila ni kuwaletea habari njema kuhusu Yesu watu wa dini ZOTE.

Yesu Kristo ndiye mahala pa kukutania kati ya Waislamu na Wakristo. Maandishi ya kale ya pekee yanayo mpa Yesu nafasi kuu sana ni ya Bibilia na Katibu kitakatifu cha Kisalmu, yaani Koran, ambayo hutaja habari za Yesu mara tisini na saba. Sura nyingi zina habari Yake. Ila tuna utofauti kadha jinsi Wakristo na Waisalmu wana mwona Yesu, bado bila swali, Yeye anasalia kuwa mtu wa faida ya pamoja na eneo la mjadala.

Epu ni wazi kuhusu msimamo wangu, Yesu alikuja kwa ajili ya dunia, hakuna dini wala desturi iliyo Yake. Yeye ana penda ulimwengu, akaufilia, na kufufuka tena, ili atoe uzima mpya kwa kila mtu. Neema Yake ni ya kila dini, ukijumlisha Waisalamu na Wakristo pamoja, Yesu ni Mwokozi wa watu wote.

Jambo la kwanza mimi uwammbia marafiki zangu Waisalamu ni, “ Mimi sijaribu kuwabadilisha kuingia katika Ukristo.” Hiyo haimainisha ya kwamba nina ona Ukristo kwa njia mbaya, ila kama iwayo yoyote, Ukristo una sehemu na shida zake. Yaani kwamba hakuna dini, halijalishi ina makusudi gani, ina uwezo wa kutufanya sisi kuwa wenye haki. Uwezo u ndani ya Yesu pekee yake. Kwa miaka nyingi nimeendelea kuonyesha Wakristo hitaji la kupokea uzima mpya kupitia Yesu Kristo. Jinsi tunavyo itikia Yesu ni jambo kuu kwa kila mtu pasipo kuweka kibao mbele cha dini. Hapo ni eneo la usawa ulio kamilika, kila mtu, mwanaume au mwanamke, Mkristo au Mwisalamu, tajiri au masikini, wanao amini na kupokea upendo wa Mungu wana Uzima wa milele.

Huduma wa maisha yangu ni kushiriki Habari njema za Yesu Kristo. Kwa miaka thelathini nimefuraihia kufanya kazi na Wakristo karibu wa madhehebu yote na katika sehemu nyingi za dunia. Mahala pa ushindani ni upendo wetu kwa watu na imani yetu katika Injili ya Yesu Kristo.

Muhammad, Koruni na Wakristo

Nikiongozea katika kufanya kazi na Wakristo, mimi kwa furaha hufanya kazi na watu wote wanao endeleza amani na ufahamu mkuu. Kusafiri kwangu kumeleta kukutana na Waislamu wengi ambao ni waaminifu, wanafanya kazi kwa bidii na watu wanao penda amani. Mara nyingi nime fanya urafiki na ufahamu kutoka kwa Waisalamu. Imekuwa ni furaha yangu kuunyosha mkono wa urafiki kwa watu wa dini zingine kuliko dini yangu, kulingani na mfano ulio tolewa na Yesu na mtume Paulo, ambao walikata kujitenga na watu wengine au makundi ya watu. Urafiki wangu na Waislamu haucha sababisha kubadili imani yangu katika Injili. Kwa upanda wengine imenisaidia mimi kulenga kiini cha ujumbe, ambaye ni Yesu na yale amefanyia ulimwengu. Tunapo geuka toka haki ya kibinafsi, na kujitegemea na kupokea Masihi aliye tumwa na Mungu ndani ua mioyo zetu, hapo tunapokea amani toka kwa Mungu. Yesu Mwenyewe ni mfalme wa Amani.

Nina kumbuka jinsi nilivyo shangazwa nilipo tambua ya kwamba Korani inazungumza kwa wingi juu ya Injili.

Nina kumbuka jinsi nilivyo shangazwa nilipo tambuwa ya kwamba Korani inazungumza kwa wingi juu ya Injili. Nabii wa kislamu Muhammad alifundisha ya kwamba Injili ina toka kwa Mungu, lakini mamilioni wa Kislamu na Wakristo wana kidogo sana au hakuna walinacho juu ya Injili. Huu ujinga una fanya kazi ya kuthirisha Habari njema kwa watu wote kuwa ya dharura sana.

Katika ziku za hapo awali za Kislamu, Muhammad alikuwa na usiano mwema na Wakristo. Wakristo na Wayahudi wana itwa kwa Kiarabu “Ahl al Kitab,” “Watu wa Kitabu”. Kurani ina leta habari njema kuelekea sisi Ahl al Kitab: Utapata ya kwamba kwa ukaribu unapo wependa walio karibu na wewe wanao jiita Wakristo, maana wao ni makuhani na waalimu katikati ya hao wasio na tabia mbaya” (Surah 5:82)

Waislamu wana himiswa kukabali Maandiko ya Wayahudi na Wakristo, na kuishi kwa amani na wao. “ Nawe usishindane na Watu wa Kitabu pasipo kuwa katika (njiani) hiyo ni mzuri, ila wao wanao tenda maovu; na kusema: Tuna amani katika yale yamefunuliwa kwetu na kufunuliwa kwenye ; Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja, na kweke Yeye tuna jisalimu” (Surah 29:46)

Nina maanisha ninapo sema ya kwamba mimi sibadilishi watu kutoka dini moja hadi ingine.

Korani inaendelea sana kusema iwapo wewe ni Mwisalamu una maswali anaweza kutafuta “Watu wa Kitabu,” “ Uliza wale wamekuwa wakisoma Kitabu mbele zako” (Surah 10:94).

Wakati wa baadaye wa maisha ya Muhammad Kurani ina nakili badhi ya ukali kati ya Waisalamu na Wakristo, pamoja na makemeo. Bado mistari zilizo nakiliwa hapo juu zina onyesha uwazi na wema. Ni vema nikiwa na lengo langu mahala ninapo sawasika, na katika kujenga daraja, kuliko yale yanayo leta mvutano zaidi. Vitabu vingi vime andikwa kuhusu vita kati ya Wakristo na Waislamu. Mtizamo wangu ni Yesu na upendo Wake kujilia wote.

Kuendeleza Yesu na sio dini

Mimi nina maanisha sana ninapo sema mimi sibadilishi watu kutoka dini moja hadi ingine. Hii inaweza kosa kuzalisha maana hukana dini inaweza kuokoa hata mtu moja. Wakristo wana kwaswa wakati mwingine ninapo sema mambo haya. Ni rahisi kwetu sisi Wakristo kuweka mtizamo watu juu ya dini ya Wakristo kuliko yule bwana Yesu. Kuangalia kwa upesi katika bibilia ita funua ya kwamba wokovu haupatakina katika kutii dini. Mistari katika Bibilia:” Yule aliye kuwa Mwana (Yesu) ana uzima wa milele haupo katika jina lingine ila jina la Yesu” weka mtizamo wako kamili kwa Yesu na Yesu pekee yake (mengi juu ya haya ni baadaye)

Nina maanisha ninopo sema mimi sibadilishi watu kutoka dini moja hadi ingine

Ili hali vile nime sema siwabadilishi watu toka dini moja hadi ingine, nina tafuta kuvuta watu wa dini zote kumkumbatia Yesu Kristo na: Haki Yake ambao ni kipawa huru kwa wote wanao amini. Hi sio kama kujaribu kumbadilisha mtu toka dini moja hadi ingine. Kwa ukweli mamilioni hudai kwamba wao ni Wakristo, na bado hawana ufahamu wa kipawa huru cha haki ya Yesu.

Urafiki, na sio mchafuko

Kama Wakristo wengi, mimi nilikuwa katika mazingira ambako Waislamu waliteswa sana. Kwa njia moja hii ilingia niani mwamgu, kwamba Waislamu walitaka kuwaua Wakristo. Na tunapo kuwa na hakuna Swala ya kwamba Waislamu wasio kuwa wa kweli wame waua Wakristo, tena ni kweli ya kwamba wanao jidai kuwa Wakristo wameua Waislamu.

Nina mawasiliano na Waisalamu wasio kuwa na mashindno au mabaya. Kwa haya na katika njia kubwa, ndiyo. Kuna na vipindi vichache ambako mchafuko yaliweza kujitokeza, lakini kila wakati Waislamu kimakosa walifikiri nina shambulia dini yao.

Kwa nini baadhi ya Waislamu wafikiri mimi ninataka kunena Kinyume cha dini yao? Wacha nieleze. Kwa miaka zaidi thelathini nimefanya mikutano mikubwa Karamu ya Injili dunia kote. Umati wa karibu 600 000 wamewahi kuwa katika ibada moja. Haku sio kila mkutano una kuwa juu zaidi, karibu kila mkutano hufika elefu kumi. Ni vigumu kufanya mkutano bila kuvutia watu wa habari. Ni katika vipindi vichache Waisalmu wamewahi kupinga matangzo yetu. Katika kila kipindi nilipo sema na Waisalmu walio weza kupinga mkutano, nilikundua kila shida ilitokana na mambo ya awali ya kushindana na Wahuburi Wakikristo. Walikuwa wame sikiza wahubiri wa Kikristo wakitumia madhabahu kudunisha Waislamu na dini yao. Walipo ona vipindi vya matangazo yetu wali dhani hiyo ilikuwa tukio lingine ambako wa Wakristo wata dunishi Waisalmu.

Nina kumbuka tukio moja kuu ambako machafuko yalitokea barabarani kwa mkutano wetu kuanza. Baada ya watu kusikia ujumbe wangu wa kwanza kuhusu Yesu watambua nilikuwa sitoi makosa Waislamu. Waisalamu kumi na tano viongozi walikuja jioni sana katika hoteli nilimokuwa. Moja baada ya moja waliniomba msamaha. Ilikuwa ni mojawapo wa nyakati za ukuso katika maishani mwangu walipo sema , “Bwana Youngren tuna tambua sasa haukuja kutu shambulia sisi wala dini yetu, ila ume zungumza kwa upendo kuhusu Bwana Yesu Kristo.”

Nilipo wezashwa kushiriki kuhusu upendo ulifunuliwa katika Yesu ni hitaji la urafiki, basi kutoelewa kuliweza kuondolewa, si maanisha tuweza kukubaliana kwa kila jambo, wala hao viongozi wa Kiaslamu walipokea Yesu kama mwokozi katika usiku huo. La, tungalia tuna tofauti, Walakini nilipo angalia upendo wa Mungu katika Yesu tulikuwa na uhiari wa kusikia.

Picha ya Mwandiko

Katika miaka za mwanzo wa 2006, magazeti za Uropa zilitoa picha za mwandiko za nabii Muhammad. Waisalmu wali ona hili kama dhihaka, na kukatokea na mandamano duniani kote. Mbaya sana ni kumba wengine wali kufa kwa ajili ya mandamano. Wakristo waka unga mkono hizo picha za mwandiko, waki sema ya kwamba ilikuwa ni uhuru wa Uwandishi. Viongozi wa Kislamu bidii kuita hizo picha kwamba ni dhihaka. Tena Wahubiri wengi wa Kikristo wakawa na shida. Wengine wakadai maandamano ya machafuko ilionyesha nyuso za kweli za Kisalamu. Nina unga mkono uhuru wa uawandishi na kwa huzuni, huu uhuru unakosekana katika inchi nyingi za Kislamu. Na bado, Wakristo wanahitaji kujua zaidi yakushambulia dini zingine. Wakati vyombo vya habari vinavyo dunisha desturi za Kikristo, huwa tuna kasirika, huwa tuna waamru vikome. Wakristo wana andamana kwa ajili ya vipindi vya kuigiza, “ Majaribio ya mwisho Ya Kristo” Ile ya DaVinci Code” maana zinadhirisha Yesu katika njia ya dhihaka kwetu. Yafaa iwe ya kwaida kuonyesha heshima kwa watu wengine. Jugumu letu la muhimu sana kuliko kukozoa au kujitetea. Wana siasia hufanya siasa. Waandishi wa magezeti haufanya kazi ya uandishi. Kuhusika kwetu sio kuongea mabaya juu ya wengine, ila ni kueneza habari njema ya yale Mungu amefanya katika Yesu Kristo kwa ajili. Nina wabishi Wakristo kuangalia jugumu letu, na Waisalmu nina wabishi wasi weze kuwa na kuogopa kuruhusu injili ya Yesu kusikika.

Vitabu vingi vime andikwa kuhusu vita vya Wakristo na Waislamu. Lengo langu ni Yesu na upendo Wake ni kwa wote.

Mimi nina Hila

Kwa wale Wakristo wanao niona kama nina hila kutaka kuwa na urafiki kati ya Waisalumu na ulimwengu wa machufuko na ukaidi, nina uliza, “ Je ni upi unafikia ulimwengu wa Wakisalamu?” Nina wauliza marafiki zangu Waisalamu wanao shambulia na kuongea maneno na mashindano juu ya Islamu, “Je ni matokeo yapi mnaona?”

La muhimu sana, ni upi mjongeleo wa Yesu? Yesu alisema, iwapo mtu wowote “ “Mimi simhukumu mtu ye yote anayesikia maneno Yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa. Yuko amhukumuye yeye anikataaye Mimi na kutokuyapokea maneno Yangu, yaani, yale maneno niliyosema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.(Yahona 12:47-48) Haya ni maneno ya ajabu.


Yesu anasema:

1. Hata hukumu yule asiye amini Yeye:
2. Kusudi ni kuleta wokovu kwa watu; na
3. Hukumu itakuja siku ya mwisho.

Je unaweza kuona vile hii ina tuweka huru ili tusi wahukumu wengine? Hi haimaanishi ya kwamba hakuta kuwepo na hukumu. La, Mungu ata hukumu kila mtu katika siku ya mwesho.

Katika kila kipindi, Yesu alipuuza hilo swala na aka lenga ujumbe Wake- kuleta wokovu na maisha mapya kwa wote bila upaguzi.

Kuna fursa nyingi leo hii ambazo zinaeleza kuingizwa katika mijadala za kisiasa Yesu pia alikumbana na janga moto hili. Mwanamke msamaria aliye ongea na Yesu alijaribu kupata shindano la ni wapi mahala pazuri pa ibaada ilikuwa katika mji wa Samaria au Yerusalemu (Yohana 4). Wafuasi wataka kujadili kuwekwa kwa ufalme wa kisiasa katika Israeli (Matendo 1:4-8) . Katika kila kipindi Yesu alipuuza swala hilo na akalenga ujumbe wake- kuleta wokovu na maisha mapya kwa wote bila upaguzi. Yesu hakuja kuhukumu, ila ni kuokoa. Tuna Yesu!

Hii nakala imetolewa kwa kitabu, “ my muslim Friends, na Peter Yongeren. Kupata nakala hii ya kitabu tembele mtandao wa gala – http://www.peteryoungren.org

Katika haya wakati mwingine ni kitabu cha kuchochea na kubisha, Wakiristo wana himzwa kukata mawazo mbaya ya kipekee ya Kislamu, ambako Waisalmu wana shawishika kujifunza zaidi ya injili ya Yesu Kristo.Yule mwandishi ananukulu kwa uhuru Bibilia na hata Kitabu kitakatifu cha Kislamu, Koran, ukitambua ya kwamba haya ndiyo maandiko ya zamani yanayo mpa Yesu nafasi kuu. Katika ulimwengu unao onekana unakaribia uharibifu, hiki kitabu kina onyesha njia ya urafiki kuliko igizo, mazungumzo badala migawanyiko. Yote zaidi yote wasomaji wata ingizwa katika kukatana kwa kilindi na Yesu “

 

 

 

 

Na: Peter Youngren

As founder of World Impact Ministries, Celebration Bible College, Way of Peace and the Celebration Churches in Toronto, Hamilton and Niagara, Canada, Peter is committed to equipping believers to fulfill their purpose before the return of Jesus Christ.

Mengi Kuhusu Peter Youngren | Nakala iliyoandikwa na Peter Youngren