Agano jipya

Na: Åge M. Åleskjær
Kutoka: October 2008
Patikana ndani ya: Lakale kushindana na agano jipya
Kila kitu ni kipya, tofauti na bora katika lile agano mpya.

Ni ya muhimu kutizimia jambo hili kwamba tuna ishi katika agano jipya, na sasa tu viumbe vipya, na tunalo amri mpya.

Agano jipya limeimarishwa kwa ahadi zilizo bora ! Tunaye kuhani mkuu aliye bora na hekalu lilo kamilika. “Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora zaidi kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi.,” (Waebrania 8:6 )

Agano la kale limejawa na ahadi nyingi zilizo kuwa mzuri, pamoja na ahadi kuhusu uponyaji, afya, maisha marefu, ustawi wa kifedha, na ushindi juu ya kila adui.Lilikuwa na ahadi kuhusu ulinzi wa Mungu na malaika wanao Linda wao,na kuhusu maombi na majibu ya maombi (Mifano Kutoka 15:26, Kutoka 23:25-26, Kumbukumbu 7:14-15, Zaburi 91, Kumbukumbu 8, na Malaki 3:10)

Hizi ahadi zote ni ndiyo katika Kristo (2 Cor 1:19-20 )

Tofauti iliyo kubwa ni hii: sasa Mungu ameheshimu hizo ahadi- ni amina ndani Yake.Na sasa ni zaidi ya hadi, zinakuwa jambo la hakika! Kila kitu tulicho haidiwa kimesha tolewa katika Kristo Yesu.( Waefesso 1:3 ) Hatuhitaji kuongejea – wakati unao kubalika ni sasa. Na ni sasa ! (2 Wakorintho 6:2 )

Na sasa hatuko tu na ahadi kuhusu uponyaji, maana kwa mapigo Yake tayari tumepata uponyaji. Na sasa hatuko tu na ahadi kuhusu kubarikiwa, tayari tumesha barikiwa na kila baraka za rohoni mbinguni, na tumefanyika tajiri kupitia umasikini Wake. ( Waefesso 1:3, 2 Wakorintho 8:9 )

Hatuko tu na ahadi kuhusu ushindi, tumebarikiwa na Yeye katika mbinguni, juu zaidi ya mamlaka na uweza na nguvu na utawala. Yeye aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yule aliye duniani.Imani yetu ndiyo ushindi ambao umeshinda ulimwengu.

Umuhimu Wa Damu

Inafaa tuelewa umuhimu wa damu yaYesu. Sababu njia ya kufikia wepo wa Mungu haikuwa wazi ni kwamba ilikuwa vigumu kwa damu ya fahali na mbuzi kuondoa dhambi. Lakini sasa Ameingia patakatifu pa watakatifu kwa damu Yake mara moja hata milele! “Kwa sadaka moja amekamilisha hata milele wale wanao takaswa.” (Waebrania 10:4)

Wakati Yesu aliposema, “hii ni damu yangu inayothibitisha agano,” (Mathayo 26:28 ), alizungumza juu ya agano jipya. Lile agano halingetenda kazi kabla ya Kalivari maana damu ilifaa ithibishe kifo cha mwenye agano.

“Wosia hauwezi kutekelezwa mpaka kumetokea kifo, kwani wosia hauna maana ikiwa mwenye kuufanya bado anaishi.” (Waebrania 9:17) Hakika damu ilifaa kuthibitisha kifo Chake ndiposa wosia ufanye kazi.

Damu ndiye msingi wa agano jipya, Ufufuo, ulio kulizaliwa upya, na yaanzisha mwanzo utu mpya, hii ilikuja kutokana na kubalika kwa damu kama dhabihu iliyo kamilika. Waebrania 13:20 yasema; “Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele.”
Tena: ufufuo ulifinyika kwa sababu ya damu! Wakati damu ilimwagika, na masharti ya Mungu ya haki ilipo timizwa, basi ufufuo ungefanyika. Hii ndiyo sababu kufanywa wenye haki haikuwezekan kabla ufufuo: “Yeye alitolewa auawe kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka ili tupate kukubaliwa kuwa waadilifu na Mungu.” (Warumi 4:25) “Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu.” (1 Wakorintho 15:17) Lakini sasa Kristo amefufuka.

Kila Kitu Ni Mpya Na Tofauti


Waraka wa Waebrania wote una husu utofauti kati ya maagano ya kale na jipya.Katika suru ya 8 Bibilia inafundisha ya kwamba agano jipya ni tofauti na lile la kale, sababu inasema ya kwamba sio kwa kadri ya lile la kale. Ni bora,na lilichukuwa mahala pake la kale.
Agano la kale lilikuwa na amri kumi yaliyo onekana: lakini agano jipya lina andikwa moyoni.
Katika agano la kale ni nabii ndiye aliye jua Bwana: lakini agano jipya “ wao wote wata nijua mimi”
Katika agano la kale tulikuwa na ukumbusho mara kwa mara kuhusu dhambi.Katika agano jipya Bwana ata wahurumia, na dhambi zao na udhalimu wa matendo yao sita ya kumbuka tena.”
Maana tuna safishwa “mara moja hata milele” “hatuna kumbusho la dhambi tena.” Waebrania 10:1-2 )
Katika agano lakale kuhani mkuu alihitaji kuwekwa mtu mahala pake baada ya kifo chake.Tulikuwa na makuhani walioweza kufanya ibada, na ilifanyika katika hema lilofanywa kwa mikono.

Katika agano jipya tuna kuhani Mkuu afanyaye katika mpangilio wa Melchizedeki, na anaye ishi milele. Yeye ni muhuduma na hekalu la ukweli,ambalo Bwana alijenga.Hapo duniani waumini wote ni makuhani kwa Mungu wetu. Sisi wenyewe ni hekalu za Roho wa Mungu, na pamoja na wengine wote tuna jengwa pamoja na tunakuwa katika hekula katika Bwana tunapo kuja pamoja katika jina la Yesu. Siye Nabii atuongozae tena.Ni Roho wa Mungu anaye ongoza watoto wote wa Mungu. (Warumi 8;14-16)

Hakuna Majengo Takatifu, Hakuna Kawaida Za Dini

Katika agano jipya, hakuna tena majengo takatifu, maana sisi tu Nyumba yake. (Waebrania 3:6 ) Sisi ndiye hekulu Lake. Yeye haishi katika majengo yaliyo tengenezwa kwa mikono ya mwandamu. Kila mitindi ikiwa na kawaida ya ibada na sala za dini, majengo takatifu,makuhani, mavazi, madhabau,mahala patakatifu na siku falani takatifu zilikuwa ni za agano la kale. Agano jipya lilianza na Ukombozi pale Kalavari.Wakati Yesu alipotolewa kama mwana kondo wetu pasaka, hii ilifanya agano la kale kufika mwisho.
Wakati wengine wanalenga Yesu alipofukuliza watu hekaluni kuwa ni jengo takatifu, hao wakati pazia ya hekaluni ilipasuka vipande tokea juu mpaka chini.Mungu akaondoka katika majengo ya mawe na kuishi ndani ya watu Wake.Nasi tumejengwa pamoja kama maskini ya Mungu katika roho. (Waefesso 2:20-22) Na sasa hekalu lilo tiwa wakfu ni sisi! Hata mwili wako ni hekalu ya Roho wa Mungu.(1 Wakorintho 6:19) Mungu anatangaza, “ nime tembeza!”

Kwa Wakristo wanao ishi chini ya agano jipya ni muhimu kuelewa sikukuu takatifu ilikuwa ni ya agano la kale. Sikukuu takatifu zimesha timilika! Ni ukatoliki ulio leta baadhi ya sherehe za siku fulani, na wakaleta na kuanzisha ibada ya bikira Maria. Pasaka ilikuwa ni picha ya ukombozi.Wakati Yesu alikuja lijitoa mwenye mara moja hata milele. Haitaji kufa tena kila mwaka.
Usi kose kunielewa mimi :mimi husherekea misa ya Kristo, Pasaka na siku ya pentakote.Lakini ninajua ya kwamba nimepewa Pasaka mwaka wote –Mungu ni Mungu aliye patanisha ! Na nina Pentakote mwaka mzima-Roho yu hapa,ina kuwa zaidi kwangu kuliko juma moja katika kalenda, haya ni mambo ya rohoni yaliyo kweli.

Kiumbe Kipya


Katika agano jipya uta tambulikana unapokuwa kiumbe kipya. Kiumbe kipya ni imani na upendo. Haihusu amri na desturi. Na tusome Wakolosai 2:16-23 : Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya Mwezi mpya au Sabato Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye Kristo. Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganifu za kidunia, na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu. Ninyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa kutoka nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:“Msishike hiki,” “Msionje kile,” “Msiguse kile!“Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu. Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima katika namna ya ibada ya kujitakia wenyewe, unyenyekevu wa uongo na kuutendea mwili kwa ukali; lakini kwa kweli, haifai chochote kuzuia tamaa za mwili.
Hapa Paulo anasema anapo kuwa mtu wa dini ni rihasi kuwa mwilini. Anasema itapandisha mwili ili uwe mtu wa dini na kusema ya kwamba vitu fulani havifai,na vitu vinafaa- usi guse, msionje,msi shike,kumbuka sabato, kumbuka sikukuu, nk Lakini mkristo amewekwa huru toka haya.Tuna ishi chini ya agano jipya.

Mashauri Pamoja Na Kuimbe Kipya Kama Mashindano


Mtume Paulo ametoa mashauri mengi kwa waumini, kuhusu tabia ya maisha na ibada. Yeye ana pinga dhambi katikati mwa Wakristo, na ana sema usile pamoja wanaoishi katika dhambi zilizo dhairi.
Lakini wakati wake wote anazungumza kuhusu kiumbe kipya. Sisi ni hekalu la Roho mtakatifu.Hii nidyo sababu tusi tanganye au tuipe nk. Ni kwa uweza wa kiumbe kipya tunawezeshwa kuishi maisha matakatifu. Waefesso 4:24. Wakol 3:10-11,Waef 2:8-10 na Wakol 2:6-10 ni mifano yake.Mwanadamu hawezi kujiokoa, na hapo hawezi kujitakasa mwenyewe!Lakini yeye aliye zaliwa upya na umejazwa na Roho,anaweza ishi maisha yaliyo juu ya kiwango mwanadamu anaye ishi kwa nguvu zake mwenyewe.

Je ni tunuku gani tunaishi katika agano jipya, baada ya Kalavari, na baada ya Pentakote

Na: Åge M. Åleskjær

Former Senior Pastor at Oslo Christian Center, now spending most of his time ministering all over Norway and internationally.

Mengi Kuhusu Åge M. Åleskjær | Nakala iliyoandikwa na Åge M. Åleskjær