Utakaso wa Kweli Kupitia Neema ya Mungu

Na: Peter Youngren
Kutoka: February 2009
Patikana ndani ya: Utakaso
Waumini hutamani kuishi maisha matakatifu na ya uungu, sasa kwa nini tunashindwa? Ni nini suluhu?

“Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi, ili kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.” (1 Wakor 1:30-31)

Mafundisho yasemayo ya kwamba sisi tu wenye haki kupitia Yesu Kristo bila sifa zetu wenyewe mara nyingi huleta mswali, “Je ni vipi tunaweza kuwa wenye haki pasipo matendo ya haki kwanza?” Tuna weza kuligeuza hili Swahili, “Ni vipi Yesu angeweza kufanyika mwenye dhambi bila kutenda matendo ya dhambi?” Kwa haya yote Bibilia inatuambia ya kwamba Yesu alipo enda msalabani Alifanya mwenye dhambi.Je hili lawezekanaje? Jawabu ni: ilikuwa ni kazi ya Mungu. Mungu alichukuwa dhambi za ulimwengu na akaweka kwa Yesu. Sisi tumefanyika wenye Haki kwa hiyo njia - ni kazi ya Mungu. Tunafanywa viumbe vipya katika Kristo Yesu bila sifa zetu wenyewe.

Wengine wanaweza kufikiri ya kwamba tuna kwepa swala la dhambi, lakini sivyo. Kwa upande mwingine, tunafundisho jinsi utakaso wa kweli huja.

Hakika Tumetakaswa

Je ni vipi tuna weza kushinda dhambi? Je ni vipi tuna takaswa? Nina taka kuonyesha kutoka kwa neno la Mungu zile nguvu za kipeke zinazo tuweka huru toka kwa dhambi na kututakasa sisi - Neema ya Mungu. Wahubiri wengine wanapenda kutumia maneno mawali yenye Paulo hataji: kwa nafasi hii na kuwa na ujuzi wa Wale walimu husema ya kuwa katika nafasi hiyo tunatakaswa katika Yesu: Yeye anakuwa hekima, haki,utakaso na ukombozi. Na wakati huo wanasema sisi ni bado pata ujuzi wa utakaso.

Yesu kwa ukweli na uhakika amefanyika utakaso wetu.

Kumbuka, Paulo anawandikia haya kwa Wakorintho, na sisi tunajua twalikuwa na dhambi na mashindano nyingi kule Korintho. Bado, Wakorintho waliambiwa, jinsi tulitamatisha jambo hii, kwamba Yesu Kristo amefanyika hekima, haki, utakaso na ukombozi. Yeye hatumia maneno kwa nafasi hii na kuwa na ujuzi wa. Yeye anaongea sana kuhusu Yesu, utakaso wetu, kama ukweli. Yesu kwa uhakika na kweli amefanyika utakaso wetu. Iwapo utakaso unakuja kwa neema, hakuna atakayo jivuna mwenyewe, ila yeye utukukaye “na ajisifu katika Bwana.” Iwapo tunaweza dai ya kwamba tunayo tu nafasi kama waliotakaswa, inakosa maana - maana tunaishi katika ulimwengu wa ujuzi. Mimi sipendi Yesu kama tu kama nafasi ya kithiolojia, ila Yesu Kristo yu ndani mwangusasa, ndani ukweli, hii ina maanisha kitu fulani. 

Dhambi imekufa

Iwapo tuanaweza kujaribu kuwa watakatifu katika uweza na nguvu zetu wenyewe, hii itatuongoza tu katika mauti.

Tuna soma, …mjihesbu nyinyi mmekufa kwa kutenda dhambi, na mu hai kwa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu”

(Waru 6:11). Tambua Paulo anasema “jihesabu”. Hii siyo katika mtizamo wa kithiolojia, lakini ni kitu kilicho halisi. Kuhesebu kitu inamaanisha kujihesabu kwa hiyo kitu. Katika maneno mengine, ni kujihesabu kwa jambo hili kwamba imekufa kwa dhambi. Anaendelea, “kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa,lakini kama mkiyaua matendo ya mwili Roho, mtaishi” (Waru 8:13). Iwapo tutajaribu kuwa watakatifu kupitia nguvu na uweza, itatuingiza katika mauti. Lakini tukijaribu mazoezi yetu kwa Agano jipya,agano la Roho lita zalisha uzima. Andiko hua, lakini Roho hutoa uzima. Tunaweza kuishi haya maisha mapya katika Kristo mradi tu tunapoweza kuruhusu Roho Mtakatifu kuwa Msaidizi wetu.

Unapo simama katika hali inayo changanyisha, tulia na umkri Yesu Kristo ni hekima yako.Hachukuwi muda mrefu. Hautaji kuomba kwa saa moja “ili upata upenyezi” au kupata upako wa hekima.”

Unapo jaribiwa kutenda dhambi, tulia na kiri Yesu Kristo kama haki yako.

Yesu Kristo ni hekima hapa na hapa.Utashangazwa jinsi hekima Yake ina jionyesha ndani mwako. Utatambuwa kwa kumwomba Yeye jawabu lita kuja pesi hata kwa hali isiyo wezakana.

Unapo jaribiwa kutenda dhambi, tulia na umkiri Yesu Kristo kama haki yako.Hauhitaji kuipigana. Unapo chukuwa muda mfupi ukikiri ya kwambo yeye ni haki yako,utambuwa jinsi gani maisha Yake yanajionyesha ndani mwako.

Ushindi haupatikana kwa kusema “LA” lakini kwa kusema ndiyo Yesu. Kwa wingi tunapo sema la kwa dhambi, ni kwa wingi tutambua dhambi. Kwa wingi tunapo sema “ndiyo” kwake Yesu, ndivyo kwa wingi tutambua Yesu, na hapo ndipo dhambi inapotesa patashika.

Ushindi haupatikani kwa kusema “LA” kwa dhambi, ila ni kusema “Ndiyo” kwake Yesu.

Utakaso wetu utulia kwake Yesu Kristo, na yale ambayo amefanya. Haitegemei wewe- inatagemea Yeye. Tazama kazi Yake iliyo kamilika.

Iwapo una jidunisha na kuona kwamba wewe haustahili, tulia na umkiri Yesu yeye ni ukombozi wako.Utatambua jinsi maisha Yake ni, nguvu na furaha yake ikidhirika ndani mwako.

“Njia za Mwanadamu”

Kunazo “njia za mwanadamu”, hata katika ulimwengu wa utakaso ulio wa kikiristo. “Mchungaji mmoja alisema iwapo una dhambi ya mazoea,una pepo mchafu.” Hivyo siye vile Agano Jipya linafundisha. Tuna soma kuhusu mtu aliyefanya mambo ambayo hakutaka kuyafanya (Warumi 7), lakini hii sura haitaji pepo mchafu. Badili yake huyu mtu anaeleza kuhusu mtu anaye jaribu kutimiliza amri za Mungu katika uweza wake mwenyewe. Kwa zaidi alipo jaribu kutimiliza Sheria katika uweza, ndivyo kwa wengi hali yake ilikuwa mbaya mno. Suluhu ya kipeke kwa haya ni “maskini” yule mtu alikuwa ni neema teletele ya Mungu. Kwa wingi tunapo mwona Yesu Kristo akifunuliwa ndani mwetu, kwa wingi ndivyo ushindi onekana maishani mwetu.

Silaha za rohoni katika Waefeso sura ya 6 inakabiliana na neema ya Mungu. Chepeo yazungumzia wokovu - tumeokaka kwa neema. Diri inalenga haki – Yesu ni haki yetu. Na mkanda ni ukweli - Yesu alisema, Mimi ndimi kweli.” Neno linazungumzia kuhusu Roho - tunaishi katika agano la Roho, na siyo la andika.Viatu vina maanisha injili ya amani - amani ambayo damu imetununulia sisi.

Nili ona kitabu kilicho kuwa na jina lake Wakristo - Mjiiweke Huru Wenyewe Je umewahi kusikia kitu kilicho na upuzi?
Je hili ndilo agano yetu? Je sisi tunaweza kujiweka huru? Wengi watajaribu, lakini wanapo jaribu kujifanya wenyewe takatifu na huru, hapo hakuwi hakika huru.Wanajiona wako huru kwa muda mfupi alafu wanaanza kutafuta uhuru tena.

Ni ya kuchulikana kutumia msemo huu “ WEWE SEMA TU LA.” Hili fundisha linasisitiza kuwa uweza nafsi yetu sisi wenyewe unatufanya kuwa takatifu. Wakati nafsi yetu inashindana na dhambi nguvu zetu zitashindwa mara nyingi.Iwapo wasia wa nguvu zetu zungezalisha utakaso, basi mauti na ufufuo wa Yesu ilikuwa kazi bure.

Sehemu Yetu

Wengi watauliza, “ Sisi tufanye nini? Hakika tunahitaji kufanya kitu?” Ndiyo ni muhimu lazima tuelewe sehemu yetu. Tu amani na kupokea yale Yesu tayari ametuandalia sisi na kumruhusu kutenda kazi ndani mwetu. Hii ni ya nguvu sana kwamba nita kupa mistari chache ya Bibilia kuunga mkono.

“Mungu mwenyewe, Mungu wa amani,awatakase ninyi kabisa, roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, nanyi mhifadhiwe kikamilifu bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.” ((1 Wathes 5:23-24).

Anaye watakasa kabisa? - “ Mungu wa amani.”

Aliye mwaminifu? -“Aliye waita

Utakaso hautegemei jitahadi letu,ila ni kazi ya Mungu ndani mwetu

Utakaso hautegemei jitihada letu ila ni kazi Mungu ndani yetu.

“Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi Yake, ili atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una Yeye milele na milele. Amen.” (Waeb 13:20-21)

Anaye tufanya wakamilifu katika kila kazi njema kafanya mapenzi Yake? - “ Mungu wa amani.”

Anaye tufanya kutenda yanayo pendeza machoni mwa Mungu? - “Mchungaji Mkuu.”

Ni vipi anatutakasa sisi? - “Kupitia damu ya agano la milele.”

Tufanye nini sasa? - Tumpe Yeye “ utakufu milele na milele.”

Kwa hivyo yote yanategemea kwake Yesu. Yeye ni haki yetu, ukombozi,utakaso na hekima.

Kwa yote inategemea Yesu.Yeye ni haki,ukombozi, utakaso na hekima yetu.

Matendo ya Mungu wakati mwingine yalikuwa ya kutisha katika agano la kale. Je unakumbuka wakati Mungu alileta mngurumo wa radi katika mlima wa Sinai? Wote wakaingiwa na wasiwasi, hata naye Musa. Sinai ilikuwa ni mfano wa utakatifu wa Mungu na ikatisha watu. Utakatifu na utakaso ulio onekana kupitia Yesu sio wa kutisha – ni wa kuvutia.

Wakati Musa alipo shuka chini katika mlima wa Sinai, watu walikimbia kwa sababu ya hofu. Wakati Yesu alipo shuka toka mlima wa mabadiliko tuna soma: “Mara wale watu walipomwona Yesu, wakastaajabu sana, wakamkimbilia Yeye, kumsalimu Yeye.” (Mark 9:15)

Utukufu wa Agano la Kale ulikuwa wa kutisha, ila utukufu wa Agano Jipya ni kuvutia.

Usije ukashusha kama mtu asipo badilishwa usiku mmoja. Mungu hakumtuma Yesu kadilisha tabia ya watu, ila ni kuwapa moyo mpya. Hapo moyo unapo badilika na tabia ita badilika pia.

Paulo anaandika, “Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema Yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, awafariji mioyo yenu na kuwaimarisha katika kila neno na tendo jema.” (2 Wathes 2:16-17)

Ataye tuimarisha katika kila tendo jema? - “Bwana Yesu Kristo Mwenyewe.” Tunapo jaribu kuwa watakatifu kupitia bidii yetu, itatuingiza katika usumbuvu na mashaka. Njia ya Mungu hutupa matokeo ya mazuri - “ufariji wa milele na tumaini jema” kupitia neema ya Mungu.”

Tumpe Yeye Utukufu

Ufunguo ni kusema “NDIYO” kwa haki, imani, upendo na amani.

Ni vipi tunaweza kuacha tamaa na tabia isiyo kuwa ya uungu? Paulo anaandika, “Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.” (2 Timoth2:22) Wengi husoma tu maneno ya kwanza nne: “Zikimbie tama za ujana.” I wapo tuna koma pale, tutashindwa. Ufunguo ni kusema “ NDIYO” kwa haki, imani,upendo na amani.

Iwapo mtoto mchanga analia, haisaidia tukisema “koma usiliye” Badili yake tutajaribu kushika umakini wa mtoto kwa kuimba, au kumtingizuia ufunguo kwake. Hapo mtoto yule anasahau kwa nini alikuwa analia katika kipindi cha kwanza! Njia ya kupata ushindi juu ya dhambi sio kwa kupigana na dhambi kupitia nguvu zetu wenyewe, ila kufauta haki, utaua, imani,upendo, uvumilivu, utu wema”(1 Timo 6:11). Tuta weza kutizama Haki ya Yesu, utaua,imani, na upendo ndani mwetu.

“Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme Wake wa mbinguni. Atukuzwe Yeye milele na milele. Amen!”   (2Timo 4:18)

Ni nani aniokoaye katika ubaya? - “Ni Bwana.” Ni nani hunilinda salama? “Ni Bwana”

Tunafanye nini? -“ Tumpe Yeye utukufu milele na milele”.

Ni nani anaye kulinda usianguke? Nina nani hukuleta bila kosa? – Mungu mwokozi wetu “

“Kwake Yeye awezaye kuwalinda msianguke na kuwaleta ninyi mbele za utukufu Wake mkuu bila dosari kwa furaha ipitayo kiasi, Yeye Mungu pekee, Mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka vina Yeye tangu milele, sasa na hata milele! Amen.” (Yuda ms 24-25)

Ni nani awezaye kuwalinda msianguke? Ni nani huleta ninyi bila dosari? - “Mungu mwokozi.”

Ni nini sehemu yetu? “Tumpe utukufu, ukuu uweza na mamlaka, vina yeye milele sasa na hata milele.”

Utakaso sio yale tunaweza kufanya, ila ni yale Yesu anafanya ndani mwetu. Kazi ni rahisi ni kuamini na kujileta sisi wenyewe Kwake. Tuna weza kuishi maisha matakatifu, walakini sio kwa nguvu zetu sisi. Utakaso wa kweli ni maisha ya Yesu ndani mwetu.

MAISHA YA YESU YANAFANYA KAZI!

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Na: Peter Youngren

As founder of World Impact Ministries, Celebration Bible College, Way of Peace and the Celebration Churches in Toronto, Hamilton and Niagara, Canada, Peter is committed to equipping believers to fulfill their purpose before the return of Jesus Christ.

Mengi Kuhusu Peter Youngren | Nakala iliyoandikwa na Peter Youngren