Maswali na Majibu yanayo husiana na...

GGN

+Ni nini Global Grace News (GGN)?

GGN (Habari za Neema Ulimwenguni) ni msaada wa mafundisho kwa wahuduma na makanisa duniani kote.Sisi tuna tangaza injili ya neema ya Yesu Kristo; neema pekee , imani pekee, Yesu pekee. Kazi ya ukombozi iliyo malizika ya Kristo ndiye toleo la pekee kwa wokovu, baraka, na huduma. Makusudi ni mawili, ni kusaidia kanisa kutambua tena Yesu na kupeleka huu ujumbe duniani kote.

+Kwa nini sasa?

Wahudumu na waamini duniani kote wanatambuwa kwamba kuna nguvu kuu dhidi ya injili leo hii; elimu ya dini, hekima ya mwanadamu na sheria zina potosha watu kutoka kwa uwazi na urahisi wa injili. GGN inataka kuwapa mafundisho, kuwa na uhusiano, na mafundisho, na kusaidia kanisa na ulimwengu kutambua yale Yesu ametupa sisi. Makusudi yetu siye yale tusiyo kuwa nayo, ila ni yale tuliyo nayo katika Kristo. Imani yetu ina tenda kazi kwa kukubali kila tendo jema katika Kristo (Phili v7).

+Je kunayo hatari ya kusisitiza zaidi kuhusu neema juu ya ukumavu wa rohoni na utakatifu wa kibinafsi?

Ufunao wa neema ni ufunuo wa Yesu na hakuna hatari ya kusisitiza ziadi juu ya Yesu. Maandiko yapo wazi waumini hutawala maishani kwa “ utele wa neema “ (Waru 5:17) na tena hiyo neema inayo tuokoa inatufundisha kuishi katika uungu (Tito 2:12). Iwapo tunataka watu waishi katika utakatifu, lazima tufunue neema ya Yesu, kwa sababu neema ndiye inazalisha utakatifu na ukomavu wa rohoni. Wale wana sumbukana na kusisitizwa kwa neema, wao huona neema ya Yesu kama kichwa cha somo lingine. Walakini, ufunuo wa neema ni ufunuo wa Yesu Mwenyewe na utakatifu wa kweli unajitokesha wakati Yesu anapoishi ndani mwetu.

+Je kuna gharama gani kupokea mafundisho haya?

Haya mafundisho yaliyopo katika mtandao wetu ni bure kwa wote. Tena unaweza kujiandikisha ili upokee barua ya habari njema ya kila mwezi iliyo bure, na tuta tuma kwa barua pepe unayo jizajili nayo. Iwapo umebarikiwa na mafundisho na unataka kuwa mshirika pamoja nasi kuendelesha mafundisho haya duniani kote, basi umekaribishwa kuwa mfadhali, yaani wa kipawa cha fedha cha wakati mmoja na hata kwa mwaka vita pokelewa na shukurani.

+Je unaona nini kwa ajili ya siku za usoni?

Tuna tarajia mapinduzi ya injili duniani kote .Ujumbe ulio hubiriwa na mitume kuhusu Yesu lazima uje mbele na nyuma na hata katikati. Kila uamsho wa kweli wa rohoni lazima uletwe na Yesu. Yesu ndiye atakaye kuwa mwongozo wa mavuno kuu yaliyo mbele zetu. Yeye ndiye “Shauku la mataifa yote” na mataifa watamjia Yeye. Makusudi ya Shetani ni kutupotosha kutoka urahisi wauliyopo ndani mwa Kristo ( 2 Wakori11:3) Huu uwongo wa Shetani huja katika mifano za ujanja chini ya kifuniko cha mambo ya rohoni na elimu ya dini. Kuna mtizamo mkubwa juu ya juhudi zetu, ina onekana kanisa lime ongezeka katika kutizama yale tunapaswa kufanya kuliko “Yale Kristo Yesu amefanya” GGN inayo nia njema kwa wahuduma na makanisa, wanao taka kanisa na ulimwengu kutambua Yesu na ukamilifu wa Kazi ya Ukombozi Wake.