Taarifa Ya Imani

Bibilia ni Neno la Mungu lilo tiwa pumzi na ni Mapenzi yaliyo funuliwa ya Mungu.

Kuna Mungu Mmoja na aliye katika utatu, kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Injili ya watu wa desturi na dini zote pasipo upaguzi.

Sisi tumepatanishwa na Mungu kupitia kifo cha Mwana Wake, ambako, Alifanya amani kwa damu Yake msalabani. Wokovu tayari umelipiwa na upo kwa kila mwanadamu. Kungali kuna hitaji la mwitikio kutoka kwa mtu kibanafsi ili kupokea kipawa cha wokovu. Mtu ana okoka kwa kukiri kwa kinywa chake kwamba Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwake kwamba Mungu alimfufua Yesu toka wafu.

Hakuna wokovu katika matendo (weponi mwa matendo mema au kutokuwepo matendo mabaya), ila tu katika Yesu Kristo.Kutubu ni kugeuka toka kuamini mambo mengine ilikfikia wokovu na kumgeukia Yesu aliye mowkozi wa pekee.

Sheria za Musa zikiwa na Amri kumi zilikuwa za Agano lilo letwa kupitia Musa.Hili agano limepata kubadilishwa na Agano Mpya lilo imarishwa katika Yesu.Sheria ya Agano jipya ni Sheria ya Upendo.

Tuna amini kikamilifu katika Neno lote la Mungu.Tuna amini yote Yesu alisema ni kweli, yote aliye yasema alipo tembea duniani hapa nay ale Aliye sema baada ya kufufuka na kuketi mbinguni.

Tume okoka kwa neema aliye bure, na hiyo neema iliyo tuokoa inwaza kubadilisha aina ya tabia na maisha yetu. Mafundisho ya haki na neema haiweki watu huru kutenda dhambi , ila ina weka watu huru kutoka kwa dhambi.

Tuna amini katika ubatizo wa maji, baada ya mtu kuja katika imani ndani ya Yesu na kumkiri Yeye kama Bwana.

Roho Mtakatifu ametolewa kwa ajili ya waaminio wote katika Yesu kama mfariji na kiongozi wa maeneo yote katika maisha.

Kila moja amepata uponyaji kupitia ukombozi wa Yesu. Kwa hivyo sisi hutia katika mazoezi maombi kw wagonjwa .